WAZIRI wa Kilimo, Mifugo na Uvuvi, Mh. Mwigulu
Nchemba, leo Desemba 14, 2015 ametembelea eneo palikozuka mapigano ya wakulima
na wafugaji wilayani Mvomero Mkoani Morogoro ambapo mtu mmoja aliuawa.
Akiandika kwenye ukurasa wake wa Facebook, Waziri alioanza kwa kusema, "Mgogoro wa wakulima na wafugaji hii leo nimefika Mvomero, kijiji cha Dihinda kata ya Kanga kufuatilia na kuchukua hatua dhidi ya tukio la mauaji, kujeruhi binadamu na wanyama lililotokea Desemba 12, 2015." Alisema, na kuongeza "Natoa rai kwa wananvhi hususan wa jamii ya wafugaji na wakulima, hakuna ardhi au mnyama mwenye thamani sawa na maisha ya mwanadamu yeyote yule, njia bora na salama ya kutatua migogoro hii
inayohusisha wakulima na wafugaji ni kufuata taratibu za kuonana na
uognozi wa serikali wa eneo husika hatua kwa hatua. " alifafanua. Waziri
alifika ili kujione uharibifu mbalimbali
ikiwa ni kuuliwa kwa mifugo.
Kadhia
hiyo iliyotokea kijiji cha Dihinda wilayani humo, tayari imepelekea kifo cha
mwananchi mmoja huku askari polisi wawili na wananchi wengine wane wakijeruhiwa.
Waziri
alishuhudia mifugo kadhaa iliyouwawa ikiwa imetapakaa kwenye eneo moja, hali
kadhalika alitembelea hospitalini kuwapa pole majeruhi.
Akiongozana
na Mbunge wa Mvomero Mh. Sadick Mourad, Mh. Waziri aliwataka wananchi hao
kuacha kujichukulia sheria mkononi.
Katika kujaribu kulitafutia ufumbuzi tatizo hilo linalojirudia mara kwa
mara, Mh. Waziri ameunda kamati za usuluhishi wa migogoro ya ardhi kwa
kila kijiji wilayani humo ambapo zitahusisha makundi yote mawili yaani
wakulima na wafugaji ili kubaini wavamizi wa maeneo na kuwachukulia
hatua haraka iwezekanavyo. Waziri alifuatana na Mkuu wa wilaya ya
Mvomero, Betty Mkwasa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269