Breaking News

Your Ad Spot

Dec 12, 2015

RAIS MAGUFULI AAPISHA BARAZA LAKE LA MAWAZIRI LEO KIPEKEE, IKULU DAR ES SALAAM

MAWAZIRI, WATEULE WARUHUSIWA KUINGIA IKULU NA WENZA WAO TU NA SIO FAMILIA




 Mh. Rais Dkt. John Pombe Magufuli, akimuapisha Mh. Angellah Kairuki, kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi na Utawala Bora, Ikulu jijini Dar es Salaam leo Jumamosi Desemba 13, 2015

Na K-Vis Media/Khalfan Said
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, ameliapisha baraza lake la mawaziri Ikulu jijini Dar es Salaam, leo Jumamosi Desemba 13, 2015.

Katika Halfa iliyofanyika ukumbi wa Ikulu jijini Dar es Salaam, mawaziri hao na manaibu mawaziri, walitakiwa kuingia ukumbini wakiwa na wenza wao tu na sio familia kama ilivyozoeleka hapo awali, ambapo kama waziri au naibu waziri ni mwanaume basi aliruhusiwa kuingia na mkewe na kama ni mwanamke aliruhusiwa kuingia na mumewe, hali iliyopelekea wale waliokuja na familia zao kuishia getini.

Hakukuwa na kupeana maua kama ilivyozoeleka na pengine ni kuogopa kile alichoonya Mh. Rais kuwa "Hakuna sababu ya kufanya sherehe kwa kuteuliwa kuwa waziri kwani kazi iliyo mbele yenu ni ngumu" alionye Mh. Rais wakati akitangaza baraza hilo Alhamisi iliyopita.

Baada ya shughuli hiyo ya kuapisha wateule hao, rais alipiga picha tatu moja akiwa na mawaziri, nyingine akiwa na mawaziri na naibu mawaziri na picha ya tatu ni ile ya baraza zima la mawaziri.

Waliokuwepo wakati wa hafla hiyo ni Makamu wa Rais, Mama Samia Suluhu Hassan, Waziri Mkuu, Bw. Kassim Majaliwa, Jaji Mkuu, Bwa. Chande Othman, Naibu spika Dkt. Tulia Ackson, na mke wa Rais Mama Janet Magufuli.

Wengine ni makatibu wakuu wa wizara pamoja na wakuu wa vyombo vya ulinzi na usalama na waandishi wa habari.

 Mh. William Lukuvi, akiapa kuwa waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
 Dkt. Hussein Mwinyi, akiapa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
 Mh. George Simbachawene, akiapa kuwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi
Dkt. Harrison Mwakyembe, akiapa kuwa Waziri wa Katiba na Sheria. Stay tune, picha zaidi zinakuja

Dkt. Augustine Mahiga, akiapa kuwaWaziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa

Mh. Charles Mwijage, akiapa kuwa Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji

Dkt. Suzan Kolimba, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na Kimataifa
Mh. Luhaga Mpina, akiapa kuwa Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, (Muungano na Mzingira)
Mh. Angelina Mabula, akiapa kuwa Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi
Mh. Injinia Isack Kamwela, akiapa kuwa Naibu Waziri wa maji na Umwagiliaji
Mh.Dkt. Medadi Kalemani, akiapa kuwa naibu Waziri wa Nishati na Madini
Mh. Selemani Said Jaffo, akiapa kuwa Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tamisemi, Utumishi, na Utawala Bora
Mh. Dkt. Ashantu Kijaji, akiapa kuwa Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages