Mwenyekiti
wa Taifa wa Shirikisho la Vyama Watu wenye Ulemavu Tanzania(SHIVYSWATA)
Amon Anastaz Mpanju akizungumza na wandishi wa habari hawapo pichani
juu ya kumpongeza Rais John Pombe Joseph Magufuli kwa kutimiza ahadi
yake ya kuyajali na kuyapa kipaumbele masuala ya watanzania wenye
ulemavu kwa uteuzi wa Naibu Waziri wa Ofisi ya Waziri Mkuu
Sera,Bunge,Kazi Vijana na Ajira Dk.Abdallah Possy, kulia ni Mwekahazina
Alias Masamaki
Waandishi
wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Taifa wa Shirikisho la Vyama Watu
wenye Ulemavu Tanzania(SHIVYSWATA) Amon Anastaz Mpanju.(picha na
Emmanuel Massaka wa Globu ya jamii).
Na Chalila Kibuda,Globu ya Jamii
SHIRIKISHO
la Vyama vya Watu Wenye Ulemavu (Shivyawata), limesema kuwa changamoto
zinazowakabili watu wenye ulemavu nchini ni ukosefu wa mazingira rafiki
ya kupatia elimu kwa jamii hiyo.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Shivyawata ,
Amon Mpanju amesema kuwa kwa serikali ya awamu ya tano iweke mkazo
katika mazingira ya watu wenye ulemavu ikiwemo na upataji wa habari kwa
kundi la watu wasiosikia.
Mpanju
amesema kuwa watu wenye ulemavu wamekuwa na sera lakini hajawahi
kutekelezwa katika serikali zilizopita hivyo kwa serikali ya awamu ya
tano itekeleze sera kwa vitendo.(VICTOR)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269