Kama ambavyo dirisha la dogo la usajili la Ligi Kuu soka Tanzania
bara linafungwa December 15, yaani siku moja imesalia kabla ya dirisha
kufungwa, barani Ulaya bado homa ya usajili wa dirisha dogo la mwezi
January inazidi kushika kasi, mengi yanaandikwa na mengi tunasikia. Mtu
wangu wa nguvu naomba nikusogezee stori 5 zilizoingia katika headlines
ya usajili December 13.
5- Mke wa Pep Guardiola ameizungumzia Man United
Klabu ya Manchester United inahusishwa kwa karibu na mpango wa kutaka kumchukua kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola kuja kuifundisha timu yao, stori ni kuwa mke wa kocha huyo amezungumza kwa mara ya kwanza kuwa anapenda kuishi jiji la Munich na sio Manchester.
4- Alex Sanchez kwenda Man City
Kwa taarifa zisizo thibitika ni kuwa uongozi wa Man City ambao pia unamtaka Pep Guardiola, unatajwa kupewa masharti na kocha huyo kumsajili staa wa Alex Sanchez kabla ya yeye hajasaini mkataba wa kuifundisha timu hiyo, kwani Sanchez yupo katika mipango yake.
3- Arsenal wanapambana na Tottenham kusaka saini ya Batshuayi
Kocha wa Arsenal Arsene Wenger anatajwa kuwania saini ya mshambuliaji wa kimataifa wa Ubelgiji anayekipiga katika klabu ya Marseille ya Ufaransa Michy Batshuayi ila kocha wa Tottenham Mauriccio Pochetino anatajwa kuwa ametenga mezani dau la pound milioni 15 ili kukamilisha dili hilo mwezi January.
2– Real Madrid wataka kumrudisha Ozil katika kikosi chao.
Ripoti kutoka Hispania zinaeleza kuwa Real Madrid wanataka kumrudisha Mesut Ozil kikosini mwao kwa njia yoyote ile endapo watamuuza James Rodriguez, Ozil aliondoka Real Madrid mwaka 2013 lakini amekuwa ni mchezaji muhimu kwa Arsenal hasa katika upigaji pasi za mwisho.
1- Man United wanafanya mipango ya mwisho ya kumshawishi kocha Pep Guardiola ajiunge na kikosi chao.
Man United wapo katika mpango wa mwisho wa kumshawishi Pep Guardiola ajiunge na kikosi chao licha ya kuwa ana husishwa kwa karibu na mpango wa kwenda kuifundisha Man City. Guardiola anadaiwa kusaini na Man City mkataba wa awali ila hajaweka hadharani bado.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269