Kaimu
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango
akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
Baadhi ya waandishi wa habari waliohudhuria katika mkutano na
Kaimu
Kamishina Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip
Mpango jijini Dar es Salam leo.
Na ChalilaKibuda,Globu ya Jamii
BAADA
ya Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa kufanya ziara ya kushitukiza katika
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na kubaini upotevu wa Makontena 329,
mapya yaibuka kwa Makampuni 43 kuhusika kukwepa kodi ya Sh.Bilioni 12.6
katika Bandari Kavu inayomilikiwa na Said Salim Bakh ressa.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo, Kaimu Kamishna Mkuu wa
Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Dk. Philip Mpango amesema kuwa
kampuni hizo 43 zilipitishiwa Kontena katika Bandari Kavu ya Said Salim
Bakhressa na kutaka ndani ya siku sita kuanzia leo kampuni zote ziwe
zimeshalipia kodi kutokana na idadi ya kontena.
Dk.
Mpango amesema katika kampuni ambazo zilizokwepa kodi ambazo
zilipitisha Kontena 329 wameshalipa zaidi ya Sh. Bilioni Tano(5) ambapo
wanatakiwa kulipa kodi iliyobaki kuweza kumaliza kodi ya Sh.Bilioni 12.6
kwa kipindi alichoweka Rais Dk .John Pombe Magufuli.
Amesema
kuwa hatilafu za kupotea kwa makontena hayo, kazi hiyo walishakuwa
wameanza kwa bahati mbaya Waziri Mkuu Kassimu Majaliwa Majaliwa
aliwawahi wakati alipofanya ziara katika mamlaka hiyo.
Kampuni
zilizokwepa Kodi ya mapato kwa makontena 329 ni Lotai Steel Tanzania
LTD yenye makontena 100,Tuff Tyres Centre Company kontena 58 Binslum
Tyres Company LTD, Kontena 33, Tifo Global Mart (Tanzania) Company
Limited Kontena 30,IPS Roofing Campany Ltd Kontena 20,Rashywheel Tyre
Center Com.Ltd Kontena 12, Kiungani Trading Company Ltd 10 Homing
International Limited Kontena 9, Red East Building Kontena Saba,Tybat
Trading Co Ltd, Kontena Tano,Zing Ent Ltd,Kotena Nne,Juma Kassem Abdul,
Kontena Tatu, Salum Continental Co.Kontena Mbili, Zuleha Abbas Ali
Kotena Mbili na Snow Leopard Building Kontena mbili na waliobaki
walikuwa na kontena moja moja.
Hata
hivyo TRA imewasimamisha kazi watu 35 wakiwemo 27 waliokamatwa katika
geti namba tano ambao hadi sasa wanashikiliwa na polisi kwa mahojiano na
uchunguzi .
Aidha amewataka wafanyakazi kuwasilisha mali zao ili kuweza kuangalia uwezo wake katika utumishi kama zinaendana na umiliki huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269