Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa
Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Na:George Binagi-GB Pazzo @BMG
Katoro alichaguliwa kuwa diwani wa Kata hiyo katika uchaguzi
uliofanyika Novemba 25,2015 kupitia Chama cha Mapinduzi CCM. Tukio hili
limejiri jana katika Mkutano wa hadhara wa CCM kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo
kwa kumchagua Katoro kuwa diwani wa Kata hiyo.
Wazee wakimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Mchungaji
Elias Lutalamamila (wa pili kulia) kwa niaba ya viongozi wa dini
akimsimika James Katoro baada ya kuchaguliwa kuwa Diwani wa Kata ya
Kayenze katika Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza.
Diwani
wa Kata ya Kayenze Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza James Katoro (CCM)
akihutubia katika mkutano wa kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa
kumchagua kuwa diwani wao. Aliahidi kushughulikia kero mbalimbali zilizo
katika Kata hiyo ambazo ni pamoja na kero ya maji, ujenzi wa zahanati
na vituo vya afya, miundombinu pamoja na ujenzi wa shule za msingi na
Sekondari.
Salum Abdallah Said ambae ni Mwenyekiti
wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa
kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika
uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Kulia ni Jeremiah Mtoni ambae ni Katibu
wa CCM Kata ya Kayenze akizungumza katika mkutano wa chama hicho wa
kuwashukuru wakazi wa Kata hiyo kwa ushindi waliokipa chama hicho katika
uchaguzi uliofanyika Novemba 25,20515.
Elias Makaranga (mwenye kinasa sauti) ambae
alikuwa Meneja Kampeni wa Diwani Katoro katika uchaguzi uliopita akizungumza
jambo katika mkutano wa kuwashukuru wananchi uliofanyika jana.
Wakazi wa Kata ya Kayenze wakifuatilia
Mkutano wa Chama cha Mapinduzi CCM katika Kata hiyo wa kuwashukuru kwa
kukichagua chama hicho katika uchaguzi uliofanyika Novemba 25, mwaka
jana.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269