Jenerali
Mwamunyange, (kulia), akiwa na Amiri Jeshi Mkuu, Rais John Pombe
Magufuli, wakati wa kufunga maonyesho ya medani jirani na kambi ya
mafunzo ya kijeshi Monduli hivi karibuni.
NA K-VIS MEDIA/
Khalfan Said
Khalfan Said
MKUU wa Majeshi
Jenerali Davis Mwamunyange, amesema Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi, Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli, amembakiza kuendelea kulitumikia Jeshi hadi Januari 30, 2017.
Jenerali Davis Mwamunyange alikuwa astaafu kazi kesho, Januari 30, 2016, baada ya kulitumikia jeshi hadi kufikia ngazi hiyi ya Mkuu wa Majeshi.
Jenerali Davis Mwamunyange alikuwa astaafu kazi kesho, Januari 30, 2016, baada ya kulitumikia jeshi hadi kufikia ngazi hiyi ya Mkuu wa Majeshi.
Jenerali Mwamunyange
aliwaambia waandishi wa habari makao makuu ya jeshi, Ngome, Upanga jijini Dar es
Salaam kuwa. “Sisi wanajeshi huwa tunabakishwa, Mh. Rais akiona anakuhitaji
kumsadia, basi muda wako wa kustaafu ukifika, wewe unabakishwa na anaweza
kukuongezea cheo, lakini mimi siwezi tena kuongezewa cheo maana hapa ndio
mwisho.” Alisema Jenerali Mwamunyange.
Tayari Mnadhimu Mkuu
mpya wa JWTZ, Luteni Jenerali Venance Salvatori Mabeyo, ambaye alikuwa Mkuu wa
Idara ya Usalama na Utambuzi ya JWTZ, ameapishwa kushika wadhifa huo mpya baada
ya mtangulizi wake, Luteni Jenerali Samwel Ndomba, kustaafu.
Majenerali kadhaa
wametaafu na tayari wengine wameteuliwa kushika nafasi zao.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269