Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu Miss Tanzania Juma Pinto akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) leo jijini
Dar-es-Salaam juu ya kujitoa kwao kama kamati ya kuratibu Miss Tanzania
ambayo ilichagulia na kampuni ya Lino International Agency, kushoto ni
Msemaji wa kamati hiyo Joketi Mwegelo na kulia ni Mjumbe wa kamati
Gladys Shao .
Msemaji wa Kamati ya Kuratibu Miss Tanzania Joketi Mwegelo akitoa maelezo kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) namna Kamati hiyo ilivyokuwa ikijitahidi kubadili mfumo ili kubadilisha muonekano wa mashindano ya urembo(Miss Tanzania) kulia ni Mwenyekiti wa kamati hiyo Juma Pinto.
Waandishi
wa habari wakimfuatilia kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya kuratibu
mashindano ya Miss Tanzania, Juma Pinto (hayupo pichani) alipokuwa
akitoa sababu za kujitoa kwa kamati katika mashindano hayo. PICHA NA Beatrice Lyimo-Maelezo.
Lilian Lundo- Maelezo,Dar es Salaam.
Kamati ya kuratibu Miss Tanzania imejitoa rasmi kusimamia mashindano ya Miss Tanzania kuanzia leo tarehe 21/01/2016.
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Juma Pinto alisema hayo leo, alipokuwa akiongea na waandishi wa habari jijini Dar-es-Salaam.
“Tumekuja
kutoa taarifa kwamba, kama tulivyo teuliwa na kampuni ya Lino
International Agency, kuandaa, kuendesha na kusimamia mashindano ya Miss
Tanzania, kamati yangu imeamua kujitoa kutokana na majukumu ya kamati
kuingiliwa na kampuni ya Lino,” alisema Pinto.
Pinto
aliongeza kwa kusema kuwa kamati yake ilipewa jukumu la kuendesha
mashindano na kuwajibika kufanya kila kitu na Lino itakuwa kama
washauri, lakini badala yake Lino imetaka kuhodhi majukumu yote na
kamati ikawa ni ya kutafuta wadhamini.
Kamati
hiyo imefanya vikao vingi vya kuhakikisha mashindano yanaboreshwa na
kubadilisha mfumo ili kuifanya Miss Tanzania kuwa na mwonekano tofauti
kama ambavyo Lino ilivyoamua kuweka kamati mpya ili kuboresha mashindano
hayo.
Kutokana
na kutopata muafaka katika vikao hivyo vya kuboresha mashindano ya Miss
Tanzania, Kamati ya kuratibu mashindano hayo kwa nia njema na wala si
kwa ubaya imeamua kujitoa katika Mashindano hayo.
Aidha,
Pinto amewaomba radhi wadhamini ambao wameshaongea nao kama kamati na
walioonesha nia ya kuwasaidia, amewataka kuendelea kufanya mawasiliano
na kampuni ya Lino kwani madhumuni ni kudhamini mashindano na sio
kamati.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269