Mkuu
wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues akisisitiza
jambo wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vya Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP) lililofanyika katika ukumbi wa NACTE,
jijini Dar es Salaam.(Picha na Philemon Solomon wa Fullshwangwe)
Na Rabi Hume, Modewjiblog
Kongamano
lililoandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO) kwa kushirikiana na Wizara ya Elimu, Sayansi,
Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi limemalizika jana jijini Dar es Salaam
baada ya kupitisha vipaumbele ambavyo vitatumika katika Mpango wa
Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP) kwa miaka mitano kuanzia 2017 –
2021.
Akizungumza
na Mo Dewji Blog, Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu,
Clifford Tandari alisema kupitia kongamano hilo wamethibitisha
vipaumbele ambavyo vitatumika ili kuifanya elimu ya Tanzania kuwa bora
na yenye manufaa kwa miaka ya mbeleni.
Alisema
kupitia kongamano hilo wamethibitisha ili kuwapo na elimu bora nchini
kunahitajika kuwa na walimu wenye sifa na ubora unaohitajika, mashuleni
kutumika vitabu vya ziada na kiada, kuimarisha huduma ya ukaguzi
mashuleni, watoto wote wenye umri wa kwenda shule wapelekwe shuleni na
kuwajengea uwezo wa stadi za kazi wahitimu ili hata wanapomaliza masomo
waweze kujiajiri.
“Tumethibitisha
yale maeneo muhimu ya sekta ya elimu ambayo tumegundua kwamba ili
tuweze kusonga mbele lazima tuimarishe ubora wa elimu yetu kama ni
walimu wasome vizuri wawe na ubora, tuwe na vitabu wanafunzi wapate
maarifa kutoka kwenye vitabu, kudhibiti ubora wa elimu na watoto waende
shule kwa shule za msingi, sekondari, vyuo vya ufundi na elimu ya juu,”
alisema Tandari.
Aidha
Tandari alieleza kuwa awali walikuwa wakishindwa kuwa na mipango ya
aina hiyo kutokana na kutokuwepo kwa fedha lakini kwa sasa wataweza
kugharamia mpango huo wa elimu kutokana na serikali kuwa tayari
kusimamia mpango huo wa kuboresha elimu ya serikali.
Aliongeza
kuwa wao kama Wizara ya Elimu wanaamini kuwa mfumo wa elimu kwa sasa
utakwenda vizuri kutokana na kasi aliyonayo rais wa awamu ya tano, Dkt.
John Pombe Magufuli ambaye ameamua kutoa elimu bure kwa wanafunzi wa
shule za msingi hadi sekondari na kutokana na kasi yake ya utendaji kazi
wanataraji utafanyika kama jinsi unavyopangwa.
Mkurugenzi
wa Sera na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari akiwaelezea
washiriki wa kongamano hilo (hawapo pichani) kuhusu Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP) ambao utafanyiwa kazi kwa kipindi cha miaka
mitano kuanzia mwaka 2017 – 2021.
Naye
Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues alisema kuwa kongamano hilo limekuwa zuri kutokana na
makubaliano ambayo washiriki wameyafikia katika kusaidia elimu ya
Tanzania kukua kwa kipindi cha miaka mitano ijayo na hiyo ni hatua ya
awali ambayo wameanza nayo na hadi kufikia mwezi Mei watakuwa
wameshakamilisha hatua zote zikiwepo bajeti na jinsi utekelezaji huo
utakavyofanyika.
Awali
Zulmira alieleza kuwa UNESCO ndiyo shirika la Umoja wa Mataifa ambalo
linasimamia elimu na wao ndiyo wameandaa mpango huo wa ESDP na
wataendelea kusaidia kukua kwa elimu nchini na hiyo ni moja kati ya kazi
wanazozifanya katika kusaidia ukuaji wa elimu na kuifanya kuwa bora
katika nchi mbalimbali ambazo shirika hilo wanafanya kazi.
Mkuu
wa Ofisi na mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), Zulmira
Rodrigues akielezea jambo katika kongamano la kujadili vipaumbele vya
Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
Mmoja
wa washiriki wa kongamano hilo akizugumza kuhusu Mpango wa Maendeleo
katika Sekta ya Elimu (ESDP), Katikati ni Mkuu wa Ofisi na mwakilishi wa
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikiaa Elimu, Sayansi na
Utamaduni (UNESCO), Zulmira Rodrigues na kushoto ni Mkurugenzi wa Sera
na Mipango wa Wizara ya Elimu, Clifford Tandari.
Mmoja
wa wanakikundi akiwaelezea wanakikundi wenzake kuhusu kipaumbele
ambacho walikuwa wamechaguliwa kukijadili na baadae kuwasilisha mbele ya
washiriki wote jinsi kipaumbele hicho kitakavyotumika pamoja na faida
zake.
Mkuu
wa kitengo cha Ushirikiano wa Kiufundi kutoka Makao Makuu ya Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO)
kutoka Ufaransa, Anton De Grauwe akimuelekeza jambo mwana kikundi
mwenzake wakati wa kongamano la kujadili vipaumbele vitakavyotumika
katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
Baadhi
ya wanakikundi wakiwa makini kufuatilia kila jambo ambalo linaendelea
katika kongamano hilo la siku mbili ili kupata vipaumbele ambavyo
vitatumika katika Mpango wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu (ESDP).
Picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269