Sheikh Hemed Jalala akizungumza jambo (aliyekaa) ni mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh Khalifa Khamis.Sehemu ya waumini wakifuatilia semina hiyo.
Sehemu ya picha zinazoonesha athari za ugaidi duniani.
Taasisi ya Kiislamu ya Imam Bukhary
Muslim Foundation jana ilifanya semina na baadhi ya waumini na wasio
waumini wa dini hiyo ili kuujuza umma kuwa ugaidi si mafundisho ya
Uslamu kama ambayo wengi wamekuwa wakidhania.
Akizungumza na wanahabari katika
katika Hotel ya Lamada, jijini Dar, mwenyekiti wa taasisi hiyo Sheikh
Khalifa Khamis amevitaka vyombo vya dola na jamii kuelewa kuwa
anapokamatwa mtu kavaa kanzu na anahusishwa na vitendo vya kigaidi
asichukuliwe kuwa ni Muislamu bali achukuliewa kama gaidi, Usilamu
haufundishi kuuwa watu.
Aidha Kiongozi wa Madhehebu ya Shia
nchini, Hemed Jalala alisema wao kama Waislamu wanaupinga vikali ugaidi
na jamii nzima inapaswa ifanye hivyo.
“Tunaiomba serikali na jamii nzima
itambue kuwa tunapinga vikali vitendo vya ugaidi na wala si mafundisho
ya dini yetu kama jinsi ilivyokaririwa, Uislamu hauna sehemu yoyote ile
inayofundisha watu wake mafunzo ya kigaidi, mauaji au vitendo vyovyote
vile vya kinyama vinavyotendeka duniani,” alisema Jalala.
(Na Gabriel Ng’osha-GPL)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269