Charles
Mombeki (Kulia) ambae ni Mkurugenzi wa International Language Training
Centre akizungumza na George Binagi kuhusiana na Umhimu wa Watanzania
kujifunza lugha za Kimataifa hususani Kiingereza kwa ajili ya kuendana
na muingiliano wa Kimataifa uliopo katika shughuli mbalimbali ikiwemo
biashara.
"Watanzania
wengi wanakosa fursa mbalimbali zilizopo. Wengine wanakosa fursa za
kibiashara pamoja na kazi kutoka katika Mashirika na Makampuni
mbalimbali duniani kutokana na kushindwa kufahamu lugha za Kimataifa
hususani kiingereza, Kijerumani, Kifarasa, Kichina na hata lugha
nyingine. Hivyo niwasihi waamue kujifunza lugha, kwa kuwa lugha
inafungua milango ya mafanikio maishani". Anasema Mombeki.
Anasema,
Watanzania wawaandae watoto wao katika lugha ya Kiingereza katika
kupata elimu, akiunga mkono shule za watu ama Mashirika binafsi kutumia
lugha ya Kiingereza kufundishia, tofauti na ilivyo kwa shule za Serikali
kutumia lugha ya Kiswahili katika kufundishia katika shule za msingi
akitanabaisha kwamba bado kiswahili hakijawa na nafasi kubwa kutumika
kimataifa kama ilivyo kiingereza ambayo ni lugha inayowaunganisha watu
wote Kimataifa.
Mombeki
anadokeza kuwa wanafunzi waliofundishwa kwa misingi ya kiingereza tangu
wakiwa wadogo wana nafasi kubwa ya kufikia malengo yao ikilinganishwa
na wale walioanza elimu yao ya awali na msingi kwa lugha ya kiswahili.
Anabainisha
kuwa kuna wanafunzi wengi kutoka Mataifa ya Afrika, Amerika na Ulaya
wanapenda kufika katika Centre hiyo ambayo ilianza kutoa elimu ya lugha
mbalimbali tangu mwaka 1998. Pia inafundisha lugha ya Kiswahili pamoja
na lugha za asili ikiwemo Kisukuma pamoja na Mila na Desturi za
Tanzania.
Imeandaliwa na George Binagi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269