Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akizungumza na raia wa China wanaoishi nchini, katika
sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa
Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika hotuba yake, Waziri
Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi
uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate
taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia
wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Kaimu Balozi wa China nchini,
Zhang Biao akizungumza katika sherehe ya raia wa China wanaoishi nchini
ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya
Golden Tulip, jijini Dar es Salaam, kabla ya kumkaribisha Waziri wa
Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) kuja
kuzungumza na mamia ya wachina hao waliohudhuria sherehe hiyo. Katika
hotuba yake, Waziri Kitwanga alisema Tanzania inatambua ushirikiano
mzuri, wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa
kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na operesheni
inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe haitagusa wenye
vibali halali.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,
Said Meck Sadick akimpongeza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (kushoto), kwa kutoa hotuba nzuri iliyowafafanulia wachina
waishio nchini kuwa Serikali ya Tanzania inawajali na inatambua umuhimu
wa ushirikiano wao uliodumu kwa kipindi cha miaka mingi, hivyo raia
yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi Tanzania, na
operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni nchini, kamwe
haitagusa wenye vibali halali. Wachina waishio nchini jana walifanya
sherehe ya kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli
ya Golden Tulip na kuhudhuriwa na mamia ya wachina hao. Kulia ni Kaimu
Balozi wa China nchini, Zhang Biao.
Raia wa China wanaoishi nchini
wakishindana kula Tunda aina ya Tikiti wakati wa Sherehe yao ya
kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden
Tulip, jijini Dar es Salaam. Katika Sherehe hiyo ambayo Waziri wa Mambo
ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga (hayupo pichani) alikuwa mgeni rasmi
ilihudhuria na mamia ya raia hao wa China. Hata hivyo, Waziri Kitwanga
alisema raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi
Tanzania, na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni
nchini, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga akiwapongeza raia wa China walioshinda mchezo wa bahati
nasibu walioucheza katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya
iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es
Salaam. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua
ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia
yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na
operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa
wenye vibali halali.
Kikundi cha Karate kinachoongozwa
na raia wa China wanaoishi nchini kikitoa burudani katika sherehe yao ya
kuukaribisha mwaka mpya iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden
Tulip, jijini Dar es Salaam. Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles
Kitwanga (hayupo pichani) ambaye alikuwa mgeni rasmi katika sherehe
hiyo, katika hotuba yake alisema nchi yake inatambua ushirikiano mzuri
wa miaka mingi uliopo kati yake na China, hivyo raia yeyote wa kigeni
anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini, na operesheni inayoendelea
ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa wenye vibali halali.
Sehemu ya raia wa China wanaoishi
nchini, wakimsikiliza kwa makini, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Charles Kitwanga (hayupo pichani) wakati alipokuwa anatoa hotuba yake
kwa Wachina hao katika sherehe yao ya kuukaribisha mwaka mpya
iliyofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Golden Tulip, jijini Dar es
Salaam jana. Waziri Kitwanga katika hotuba yake alisema nchi yake
inatambua ushirikiano mzuri wa miaka mingi uliopo kati yake na China,
hivyo raia yeyote wa kigeni anatakiwa afuate taratibu za kuishi nchini,
na operesheni inayoendelea ya kuwakamata raia wa kigeni, kamwe haitagusa
wenye vibali halali.
(Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269