Jana
wakimbizi kutoka katika kambi za Nyarugusu na Nduta zilizopo mkoani
Kigoma waliungana na watu wengine ulimwenguni kuadhimisha siku ya maji
duniani ambapo kauli mbiu ya mwaka huu ni maji safi kwa maendeleo
endelevu.
Maadhimisho
hayo yaliandaliwa kwa ushirikiano kati ya serikali kupitia idara ya
wakimbizi na mashirika mbalimbali yanayotoa misaada katika makambi hayo
yakiwemo UNHCR, UNICEF, International Rescue Committee, Oxfam, TWESA,
Save the Children, Water Mission, TCRS na mengine mengi.
Maadhimisho
hayo yalipambwa na burudani mbalimbali zikiwemo ngoma na maigizo na
kisha risala zilizosisitiza umuhimu wa kutunza vyanzo vya maji.
Kwa
mujibu wa shirika la kuhudumia wakimbizi UNHCR hadi sasa kuna wakimbizi
kutoka mataifa mbalimbali zaidi ya 140,000 wanaoishi katika kambi ya
Nyarugusu huku katika kambi ya Nduta kuna wakimbizi takribani 50,000
kutoka Burundi.
Tangu
kufunguliwa tena kwa makambi hayo mwaka jana, mashirika mbalimbali
yamekuwa yakitoa misaada ya kibinadamu katika makambi likiwemo shirika
la Oxfam ambalo linatoa huduma za maji na ujenzi wa vyoo ikiwa ni pamoja
na kuwafundisha wakimbizi namna mbalimbali za kuishi kwa kuzingatia
kanuni bora za afya ili kujilinda dhidi ya magonjwa.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269