Breaking News

Your Ad Spot

Apr 4, 2016

KAMATI YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII YATEMBELEA HOSPITALI YA TAIFA MUHIMBILI, TAASISI YA TIBA YA MIFUPA, MISHIPA YA FAHAMU NA UPASUAJI WA UBONGO NA TAASISI YA MOYO YA JAKAYA KIKWETE DAR ES SALAAM LEO

Mbunge wa Bunda (V) Boniface Getere, (wa kwanza kushoto) akizungumza jambo wakati wa Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii ilipotembelea moja ya chumba wanacholala wagonjwa wenye matatizo ya watu wenye upungufu wa akili katika Hospitali ya Taifa Muhimbili. (PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)


Dk. Frola Lwakatare wa kitengo cha mionzi cha Muhimbili akitoa maelezo ya kitaalam kwa wajumbe wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii waliotembelea hapo



Kaimu Mkurugenzi wa Fedha na Ugavi wa Moi Kulwa Malendeja akimsalimia na kumkaribisha Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba alipotembelea Taasisi ya Tiba ya Mifupa na upasuaji, Ubongo na Mishipa ya Fahamu Muhimbili (MOI)

Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa Moi, Dr. Othman Kiloloma akiwasilisha ripoti ya Kiutendaji ya mwaka
Mbunge wa Viti Maalum Vyuo Vikuu na Mkuu wa Wilaya Dodoma, Dr. Jasmine Tiisekwa akizungumza jambo wakati wa Kamati ya Bunge ilipo tembelea Muhimbili, Moi na Taasisi ya Jakaya Kikwete  





Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Hospitali ya  Muhimbili, Profesa. Lawrence Museru akitoa maelezo ya kina namna Hospitali hiyo ya Taifa inavyojiendesha na changamoto zake.
 Waziri Kivuli wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi , Susan Lyimo akizungumza jambo wakati wa Kamati hiyo ya Bunge ilipotembelea Hospitali ya Taita ya Muhimbili,   Taasisi ya Mifupa na Mishipa ya Fahamu na Upasuwaji wa Ubongo Moi na Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete Jijini Dar es Salaam leo.
Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Maendeleo ya Jamii, Peter Serukamba akisaini kitabu cha wageni Moi, wakati kamati hiyo ilipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili,  na Taasisi ya Jakaya Kikwete


Mbunge wa Jimbo la Ilala na Mjumbe wa Kamati ya Bunge Mussa Zungu akizungumza jambo wakati wa majumuisho ya Kamati hiyo ilipotembelea Hospitali ya Taifa Muhimbili, Taasis ya Tiba Moi na Taasisi ya Jakaya Kikwete Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages