Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu (wa pili kulia), akikata utepe kuashiria uzinduzi rasmi wa
Taasisi ya Basila Mwanukuzi (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation)
yenye lengo la kusaidia wanawake kuinua uwezo wao wa kibunifu ili
kujiinua kiuchumi hasa Mama Lishe kwa kushirikiana na wadau mbali
mbali. Uzinduzi huo umefanyika leo Aprili 11, 2016 kwenye Ukumbi wa
Makumbusho ya Taifa, Jijini Dar es salaam. Wengine pichani ni
Mwanzilishi wa Taasisi hiyo, Basila Mwanukuzi (kulia), Kaimu Mkurugenzi
wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja pamoja na Mwakilishi wa Mama
Lishe, Bi. Grace Foya.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu akizungumza na wageni waalikwa wakati wa uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es salaam.
Basila Mwanukuzi Mkurugenzi wa Taasisi ya (Basila Mwanukuzi Empowerment Foundation) akimkaribisha Waziri Ummy Mwalimu ili kuzungumza na wageni waalikwa na kisha kuzindua rasmi taasisi hiyo.
Baadhi ya ndugu na wanafamilia wa Basila Mwanukizi wakiwa katika hafla hiyo
Mrisho Mpoto kushoto na Miriam Ikoa mmoja wa waliowahi kuwa Miss Tanzania wakiwa pamoja na wageni wengine katika hafla hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu akisalimiana na Basila Mwanukuzi mara baada ya kuwasili katika uzinduzi huo Katikati ni Kaimu Mkurugenzi wa Maendeleo ya Jinsia, Timoth Mgonja
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu akisalimiana na baadhi ya akina mama Lishe waliohudhuria katika hafla hiyo ya uzinduzi.
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia matukio katika hafla hiyo.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Miss Tanzania Hashim Lundenga.
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy
Mwalimu na Basila Mwanukuzi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269