Na Ripota wa Sufianimafoto Blog,Dar
UKIHADITHIWA
na kuonyeshwa chumba cha Dereva Tax anayeonekana kitaani na katika kazi zake akiwa
amepiga pamba wala hutaamini masikio yako wala macho yako pindi utakapopata
bahati ya kufika na kushuhudia chumba hicho kilichopo maeneo ya Gold Star Mtaa
wa Mbezi Mtoni Bondeni jijini Dar es Salaam.
Mtandao
huu ulipata fursa ya kufika na kushuhudia yale yaliyokuwa yakisemwa na baadhi
ya wakazi wa mtaa huo jana majira ya saa tano usiku baada ya kutokea mtafaruku
na sintofahamu katika nyumba hiyo ya Mama Mwakajinga, anayoishi Dereva huyo
aliyejulikana kwa jina la Steven al-maarufu kama 'NYATI'.
Akizungumza
na mtandao huu wa Sufianimafoto, Mama mwenye nyumba kuhusu tukio hilo, alisema
kuwa siku ya Mei 23, akiwa ameketi uwanji karibu kabisa na Chumba cha Jamaa
huyo huku akichambua mboga, alihisi harufu kali na mbaya iliyokuwa ikivuma
kutoka chumbani kwa Dereva huyo aliyepanga katika nyumba yake tangu mwaka 2008
na kuona wadudu aina ya funza wakitoka chumba hicho kupitia chini ya mlango.
Kesho
yake Mei 24 Baada ya kuona wadudu hao huku harufu ikizidi kuwa kali, alimuita
jirani yake na kumshirikisha jambo hilo huku wote wakishikwa na butwaa na kuwa
na mashaka na chumba hicho.
Mei
25 Mama mwenye nyumba aliamua kwenda kwa Mjumbe wa eneo hilo Badili Makoye,
kutoa taarifa juu ya wasiwasi uliotanda katika nyumba hiyo na kuongozana na
Viongozi wengine, Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa huo, Frank Kyaruzi, Wajumbe
wengine Abdalla Mlaliya na Matrida Paston, waliofika na kujionea hali
halisi ya chumba hicho.
Baada ya viongozi hao kufika eneola tukio walimuamuru
Mama mwenye nyumba kwenda kutoa taarifa kituo cha Polisi. Mama huyo
alitekeleza agizo na kwenda kuripoti Kituo cha Mbezi Garden na kuongozana na
Mkuu wa Kituo hicho na baadhi ya askari hadi nyumbani na kukuta hali hiyo ya
sintofahamu.
Walipofika eneo la tukio na kushuhudia hali hiyo, Mkuu
wa Kituo aliamuru mlango huo uvunjwe huku wanachi na Viongozi wa Mtaa huo
wakishuhudia na kuingia ndani ambako walikuta Chumba kizima kikiwa kimejaa
Chupa za Plastiki zilizojaa mikojo, Mifuko ya Rambo ikiwa na Vinyesi, Feni moja
iliyochomekwa kwenye Soketi ya Umeme ukutani, Pakiti nyingi tupu za Sigara aina
ya Embassy na Kondomu zilizotumika na zisizotumika.
Baada
ya zoezi hilo, Mwenyenyumba alimpigia simu mpangaji wake na kumtaka kurejea
nyumbani, lakini Dereva huyo alijibu kuwa kwa muda huo alikuwa mbali maeneo ya
Kunduchi na kuahidi kuwagongea usiku pindi atakaporejea.
Hadi Mtandao huu unaondoka eneo la tukio majira ya saa
tano usiku bado wakazi wa maeneo hayo walikuwa wamejazana nje ya Chumba hicho
wakiendelea kumsubiri arudi ili kupata ukweli kuhusu mambo waliyoyaona katika
chumba chake.
Aidha Mama mwenye nyumba aliuambia mtandao huu kuwa
mpangaji wake huyo, tangu alipohamia katika nyumba hiyo mwaka 2008, hakuwahi
kumuona akiingia na mwanamke katika chumba hicho, wala kumuona mgeni wa aina
yeyote kwa Dereva huyo,jambo lililomshangaza kukuta Kondom zilizotumika katika
chumba hicho. Ama kweli ukistaajabu ya Mussa utayaona ya Filauun.
Hadi leo hii Mei 27, mtandao huu umeshindwa kumpata
dereva huyo baada ya kutompata hewani simu yake ikiwa imezimwa tangu kutokea
kwa tukio hilo.
Leo hii Mei 27, Mama mwenye nyumba ameripoti kuwa
mpangaji wake huyo,hajatokea nyumbani hapo tangu kutokea kwa tukio hilo ambapo
leo, amechukua uamuzi wakuwalipa vijana wa mtaa huo ili wasafishe chumba hicho.
Tayari tumewalipa pesa vijana kiasi cha sh.200,000/=
ili wafanya usafi na wameshamaliza na kwenda kufukia bonde la mto Mbezi
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269