Mkurugenzi
wa Azam Media Tido Mhando (Kushoto) akizungumza wakati wa uzinduzi wa
Maisha Plus East Africa Mkurugenzi wa Maisha Plus East Africa msimu wa
5 ambapo shindano linatarajiwa kuanza hivi karibuni itakapotangazwa
ratiba ya kutafuta washiriki wa shindano hili mikoani na nchi zingine za
Afrika Mashariki, kulia ni mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw.
Masoud Kipanya, Masoud Kipanya ni miongoni mwa waanzilishi wa Maisha
Plus na mtangazaji wa kipindi hicho ambacho huandaliwa na kampuni ya
DMB Company Limited na mwaka huu inandaa kwa udhamini mkubwa wa Azam
Media, Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika jana katika studio za Uhai
Productions – Azam, Tabata jijini Dar es salaam.
Joyce
Fisoo Katibu Mtendaji wa bodi ya filamu Tanzania akizungumza mawili
matatu wakati wa uzinduzi huo kama mgeni mwalikwa lakini pia kama mdau
muhimu wa shindano hilo.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika hafla hiyo
Mmoja wa waandaji wa shindano hilo Bw. David Seburi akizungumza na baadhi ya wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo.
Baadhi ya waandaji wa shindano la
Maisha Plus kulia Francis Bonga na David Sevuri wakifuatilia matukio
wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.Jikho Man na Vitalis Maembe wakitoa burudani wakati wa hafla hiyo iliyofanyika jana.
Mwandaaji
wa shindano hilo Bw. Masoud Kipanya akizungumza na baadhi ya washiriki
waliowahi kushiriki katika shindano hilo kulia ni Abdul aliyekuwa
mshindi.
Aliyewahi kuwa mshindi wa shindano hilo Abdul akizungumza na wageni waalikwa katika uzinduzi huo uliofanyika jana.
Baadhi ya wafanyakazi wa Azam Media wakiwa katika hafla hiyo.
Mwanahabari
na Bloger John Bukuku akihojiwa na mtangazaji wa Azam Tv Benerick
ambaye pia alikuwa ni mmoja wa washiriki wa msimu uliopita wa Maisha
Plus.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269