Mzunguko (Roundabout) na Stesheni kuu ya reli Kigoma. (Picha na K-VIS MEDIA/Khalfan Said) |
NA K-VIS MEDIA
MKOA wa Kigoma umekaukiwa na sukari kuanzania Ijumaa Mei 20,
2016 na taarifa ya Ofisi ya Biashara ya Mkoa, imesema, Wakazi wa Manispaa ya
Kigoma –Ujiji wavumilie hadi mwisho wa mwezi huu wa Mei.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka mkoani humo, kabla ya siku ya
Ijumaa, sukari iliuzwa kwa bei ya shilingi elfu 5,000 kwa kilo, kwenye eneo la
Manispaa ya Kigoma-Ujiji, lakini Ijumaa maeneo yote ya manispaa hiyo hayakuwa
na sukari hata hiyo ya shilingi elfu 5.
Akizungumzia uhaba huo mkubwa wa sukari mkoani humo, Afisa
biashara wa mkoa wa Kigoma Deogratius Sanga, amekiri kuwepo kwa uhaba huo na
kuwataka wananchi wa Manispaa hiyo kwua wavumilivu wakati serikali ya mkoa
inatafutia ufumbuzi tatizo hilo. “Taarifa toka bodi ya sukari ni kwamba ile
sukari iliyoahidiwa na waziri mkuu itafika mwisho wa mwezi huu, na tunategemea
kuanzia mwezi ujao tatizo hili litakwisha”.alisema Sanga
Bandari ya Kigoma
Mwalo wa Kibirizi |
Manispaa ya Kigoma- Ujiji
Uwanja wa Lake Tanganyika
Khalfan Said
Chief Photographer/Owner
K-VIS MEDIA
P.Box 77807
Mobile; +255 646-453/+255-653-813-033
Office; Mivinjeni Opp.Tanesco, Kilwa RD
Blog:http//khalfansaid.blogspot.com
Dar es Salaam, Tanzania
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269