Breaking News

Your Ad Spot

May 23, 2016

WIZARA YA AFYA YATANGAZA NAFASI ZA AJIRA 192 KWA DHARURA, MWISHO WA KUTUMA MAOMBI JUNI 6, 2016


Waziri wa Afya, Mh. Ummy Mwalimu
  
NA K-VIS MEDIA/Khalfan Said
WIZARA YA Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imetangaza nafasi za ajira 192 kwa dharura, kwa wataalamu wa fani mbili za afya ambazo ni Tabibu wasaidizi (Clinical Assistant), nafasi 95 na Wauguzi (Enrolled Nurses) nafasi 97.

Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara hiyo iliyotolewa leo Jumatatu Mei 23, 2016 na kusainiwa na Katibu Mkuu wa wizara, Iimeeleza kuwa Wizara imeridhia mpango wa ajira ya dharura ili kukabiliana na uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika sekta hii. “Mpango huu utaendeshwa kwa Fedha za mfuko wa CDC (Centre for Disease Control) Awards No. 5U2GGH001062-03 kwa mwaka wa Fedha ulioanzia Aprili 2016 kwa muda wa miaka miwili. “Taarifa hiyo imefafanua.

Watumishi watakaopata ajira kupitia mradi huu watapangiwa vituo vya kazi vilivyoko katika maeneo yenye uhaba mkubwa wa watumishi husika na ambayo mazingira yake ni magumu, taarifa hiyo imeendelea kusema.

Taarifa hiyo ya wizara imeendelea kufafanua kuwa watumishi hawa baada ya kumaliza mkataba wao, wataingizwa katika ajira za serikali kulingana na upatikanaji wa vibali vya ajira kwa mwaka husika.

Wizara imewataka wote wenye nia ya kuomba watume maombi yao yakiwa yameambatanishwa navivuli vya vyeti vya kumaliza kidato cha nne, cheti cha taaluma pamoja na leseni, (kwa wauguzi)
Taarifa kamili soma hapo chini


JAMHURI YA MUUNGANO YA TANZANIA
WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO

AJIRA YA DHARURA KATIKA SEKTA YA AFYA
UTANGULIZI
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imeridhia mpango wa Ajira ya dharura kwa wataalamu wa fani mbili za afya. Mradi huu umelenga kuchangia juhudi za serikali katika kukabiliana na uhaba mkubwa wa wafanyakazi katika sekta hii. Mpango huu utaendeshwa kwa Fedha za mfuko wa CDC (Centre for Disease Control) Awards No. 5U2GGH001062-03 kwa mwaka wa Fedha ulioanzia Aprili 2016 kwa muda wa miaka miwili. Watumishi watakaopata ajira kupitia mradi huu wanakadiriwa kuwa 192 na watapangiwa vituo vya kazi vilivyoko katika maeneo yenye uhaba mkubwa na ambayo mazingira yake ni magumu. Watumishi hawa baada ya kumaliza mkataba wao, wataingizwa katika ajira za serikali kulingana na upatikanaji wa vibali vya ajira kwa mwaka husika. Watumishi hawa ni kama ifuatavyo: Tabibu Wasaidizi (Clinical Assistant) 95 na Wauguzi (Enrolled Nurses) 97. Maombi yote yaambatanishwe kivuli cha cheti cha kumaliza kidato cha nne, cheti cha taaluma pamoja na leseni (kwa wauguzi)
MSHAHARA NA MASILAHI
Mshahara (kwa kiwango cha juu cha mshahara wa kila fani husika)
Posho ya kujikimu ya siku saba za mwanzo
Bima ya Afya ya asilimia 3%
Kiinua m,gongo cha asilimia 25% ya mishahara baada ya miaka (2);
Malipo ya pango ya asilimia 30% ya mshahara
Nafasi ya kupatiwa mafunzo elekezi.

Mwisho wa kupokea maombi ni tarehe 06/06/2016, Maombi yote yatumwe kwa njia ya posta:-

Katibu Mkuu
Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
S.L.P 9083
6 Samora Machel Avenue, 11478
Dar es salaam, Tanzania

2 comments:

  1. Sawa, pia vipi kuhusu ajira za wauguzi wengine tuliopata leseni zetu mwezi wa saba mwaka huu? mbona bado hatujapangiwa vituo vya kazi?

    ReplyDelete
  2. Sawa, pia vipi kuhusu ajira za wauguzi wengine tuliopata leseni zetu mwezi wa saba mwaka huu? mbona bado hatujapangiwa vituo vya kazi?

    ReplyDelete

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages