Anaitwa Devota Sotel kutoka 91.0
Passion Fm Mwanza. Kwa muda mrefu amekuwa king'ang'anizi katika umahiri
miongoni mwa watangazaji bora wa vipindi vya taarabu Jijini Mwanza na
hata Kanda ya Ziwa.
Mambo yake si ya kitoto ukimsikiliza
katika kipindi cha "Ambaa na Mwambao" kinachoruka 91.0 Passion Fm Mwanza
kila siku jumatatu hadi ijumaa kuanzia saa tano asubuhi hadi saa nane
mchana.
Lakini pia jumamosi kuanzia saa tisa
alasiri hadi saa kumi na mbili jioni na jumapili kuanzia saa kumi na
moja jioni hadi saa mbili usiku.
Uwepo wake katika tasnia ya
utangazaji hususani katika vipindi vya taarabu, kumeibua watangazaji wa
taarabu wapya Mwanza ambao wamekuwa na ndoto za kufanya kazi kwa juhudi
zaidi ili kumtoa Devota kwenye ubora wake alioukomalia kwa miaka mingi
sasa.
Wapo watangazaji wengi wa taarabu
ambao wanaibuka kwa kasi ya ajabu Jijini Mwanza na hivyo kuongeza mvuto
kwa mashabiki wa taarabu Mwanza ambao wamekuwa wakipata wakati mgumu ni
mtangtazaji yupi wamsikilize na ni yupi wamuache.
Ubunifu pekee ndio utakaobainisha nani bora zaidi kwa mwaka huu 2016 na hivyo kumuondoa Devota kwenye ubora wake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269