Kampuni ya ChemicotexCotex wazalishaji
wa dawa ya meno aina ya Whitdent, imefanya sherehe kubwa ya kutimiza
miaka 25 tangu iingie sokoni kwenye hoteli ya Serena jijini Dar es
Salaam, Julai 9, 2016.
Katika sherehe hiyo ambayo mgeni rasmi
alikuwa Katibu Mkuu wizara ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
(Anayeshughulikia viwanda), Dkt. Adelhem Meru, imezindua promosheni
kamambe ambapo jumla ya magari mapya 25 yatashindaniwa. Pichani msichana
mrembo akiwa amesimama mbele ya magari hayo wakati wa uzinduzi wa
promosheni hiyo. (PICHA NA ALLY DAUDI-MAELEZO)
Dkt. Meru akionyesha boksi la dawa ya Whitedent wakati wa sherehe hiyo
Dkt. Meru akitoa hotuba yake
NA
ALLY DAUDI-MAELEZO
Tanzania
inatarajiwa kufikia uchumi wa kati kufikia mwaka 2020 kwa kutumia sekta ya
viwanda vikubwa, vya kati na vidogo ili kupiga hatua katika maendeleo ya nchi.
Akizungumza
hayo hafla ya kutumiza miaka 25 ya dawa ya meno ya whitedent iliyofanyika leo
jijini Dar es salaam Katibu Mkuu wa Viwanda,Biashara na Uwekezaji Dk. Adellhem Meru amesema kuwa wameweka mkakati na
malengo ya kukuza uchumi wa kati kwa kutumia Mchango wa viwanda.
“Mpaka
kufikia mwaka 2020 lazima tufikie uchumi wa kati kutokana na Sekta ya viwanda
ili tuweze kuendelea na kupata pato la taifa kutoka
asilimia 7.5 mpaka asilimia 15 na kuwa na uchumi imara kama Watanzania”
alisisitiza Dkt. Meru.
Aidha
Dkt. Meru amesema kuwa katika malengo waliyojiwekea kwa serikali ya awamu hii
ni kuhakikisha mpaka mwaka 2020 ajira nyingi zitatokana na viwanda kufikia
asilimia 40 na kuendelea.
Katibu
Mkuu huyo ametoa rai kwa watanzania kwa kuwataka wwapende zaidi kutumia bidhaa za viwanda vya nyumbani kuliko
kupendelea bidhaa zinazotoka nje ya nchi.
Mbali
na hayo Dkt. Meru aliwapongeza kiwanda kinachotengeneza dawa ya meno ya
Whitedent Chemi & Cotex kwa kutimiza miaka 25 tangu waanze kuzalisha bidhaa
hiyo na kuwataka waendelee na uzalishaji wao kwa miaka 25 ijayo.
Kwa
upande wa Afisa mkuu wa Chemi & Cotex Bw. Raja Swaminathan alisema kuwa
katika kusheherekea miaka 25 ya bidhaa yao wametaka kuwashirikisha watanzania
kwa kutoa magari 25 ili yashindaniwe na wananchi wote kwa miezi mitatu.
“Tungependa
kila mtu awe na nafasi ya kushiriki katika mafanikio yetu kwa kucheza shindano
hili kwa sababu bidhaa hii ni mali ya watanzania na inatengenezwa Tanzania “
alisisitiza Bw.Swaminathan.
Wafanyakazi na wageni waalikwa wakiwa kwenye hafla hiyo
Dkt. Meru akiteta jambo na Mkuu wa Operesheni wa CHEMICOTEX, Raja Swaminathan
Dkt. Meru akilishwa keki ya maadhimisho ya miaka 25 ya Whitedent kuwa sokoni
Dkt. Meru, akikaribishwa na wenyeji wake wakati akiwasili ukumbini
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269