Kamanda
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP),
Simon Sirro akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari ofisini
kwake Dar es Salaam leo, wakati akitangaza kiama kwa mwananchi yeyote
atakayefanya maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania
yaliyoandaliwa na Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema).
Kamanda Sirro akisisitiza jambo kwenye mkutano huo.
Magari
ya polisi yenye zaidi ya askari 80 yakiondoka Kituo cha Polisi cha
Kati, yakielekea Vikindu kwa ajili ya Operesheni saka majambazi.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Askari
wa kikosi maalumu cha kupambana na uhalifu wakiondoka Kituo Kikuu cha
Polisi cha Kati kuelekea Vikindu kwa operesheni maalumu ya kuwasaka watu
wanaotuhumiwa kwa ujambazi.
Na Dotto Mwaibale
KAMANDA
wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Kamishna wa Polisi (CP),
Simon Sirro ametangaza kiama kwa mwananchi yeyote atakayefanya
maandamano Septemba Mosi ya kupinga udikiteta Tanzania yaliyoandaliwa na
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema)
“Jeshi
la polisi mkoa wa Dar es Salaam tumejipanga vizuri siku hiyo nawaomba
wananchi wasidhubuti kujitokeza kuandamana siku hiyo kwani watakiona cha
moto” alisema CP Sirro.
Sirro
alisema tayari jeshi hilo lina taarifa za kiinteligensia kuwa kuna
vijana wanapewa fedha kwa ajili ya kuandamana na kufanya fujo Septemba
mosi.
Aliwasihi wananchi hasa vijana kutoingia barabarani Septemba mosi na kuwaachia wachache wenye nia ya kuletafujo.
“Ni
rai yangu wale wananchi wazalendo wan chi hii wasiopenda kupambana na
jeshi lao la polisi ambalo linawalinda na kulinda mali zao siku hiyo
wasiingie barabarani,” alisema.
Aliwakaribisha
wanao taka kuingia barabarani na kupambana na jeshi hilo na kuwa
watakamatwa na kufikishwa kwenye mkono wa sheria.
“Sisi
tupo vizuri na tupo imara hasa kwa wale wanaopenda kuvunja sheria kwa
makusudi wata wajibika kwa mujibu wa sheria, hivyo suala la utiiwa
sheria bila shuruti ni la msingi sana,” alisema Sirro.
Alisema
jeshi hilo limejiandaa kwa wananchi wachache ambapo alibainisha
wananchi wengine hawana haja na maandamano hayo huku akibainisha vijana
wachache wenye shida kupewa fedha na viongozi kwa lengo la kuandamana.
“Jiulize
hiyo 40,000 unayo pewa kuingia barabarani na matokeo yake ukavunji
kama mguu hiyo 40,000 ina thamani gani kwani… kwa hiyo mimi kama
kiongozi wenu wa jeshi la polisi na sisitiza na ninaelekeza tuwaache
wale wenye sababu zao binafsi waingie barabarani,” alisema.
Katika
hatua nyingine Kamanda Sirro alisema askari zaidi ya 80 wa kikosi
maalumu cha kupambana na uhalifu wameondoka kwenda vikindu na maeneo
mengine wilayani Mkuranga mkoani Pwani kufanya operesheni ya kuwasaka
watu wanaodhaniwa kujihusisha na ujambazi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269