Nijioni
ya leo Agosti 21, 2016, kuona kituo cha Daladala kuwekwa chini ya
Daraja la Treni lililopo Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam, kama
inavyo onekana Pichani ni gari ya Abiria maarufu Daladala linalofanya
safari zake kati ya Mbagala rangi tatu na Buguruni lenye namba za
Usajili T 233 CUY, likiwa limeegesha chini ya Daraja la Treni lililopo
maeneo ya Mtoni Mtongani ambapo haikufahamika mara moja Abiria hao
walikuwa wametoka wapi wakionekana kwa wingi wakiingia katika gari hilo
ambapo nihatari kwa abiria hao na mali kwa ujumla, nijambo la
kusikitisha kwa dereva aliyepitia mafunzo na kufanya kituo hapa na kama
inavyo fahamika ni Barabara kubwa na magari huwa yakipita kwa kasi
yanapoteremka mteremko huo wa kuelekea Mbagara rangi tatu, alaumiwe
nani ? mazowea nikama sheria nikiwa naimani wahusika watachukua hatua
kali na kutowa fundisho kwa wengine na leseni zao kuondolewa barabarani
na watangwazwe wazembe wote watakao kuwa wazembe na watakao sababisha
ajali.
Abiria
wakipanda eneo hilo hatarishi katika mteremko uliopo chini ya Darala la
Treni maeneo ya Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam bila ya kujili kama
sehemu hiyo si salama
Abiria wakipanda
Pichani
ni Gari lenye namba za Usajili T 951 CDZ, linalofanya safari zake kati
ya Temeke na Kongowe nalo likipakia Abiria eneo hilohilo lililopo chini
ya Daraja la Treni, Mtoni Mtongani Jijini Dar es Salaam
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269