Rais Mstaafu Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakionyesha cheti chao cha Jubilei ya dhahabu ya miaka 50 ya ndoa yao |
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu Benjamin William Mkapa Agosti 27, 2016 ameadhimisha Jubilei ya Dhahabu ya Miaka 50 ya ndoa yake na Mama Anna Mkapa katika Kanisa la Mtakatifu Petro, lililopo Oysterbay Jijini Dar es Salaam.
Misa ya Jubilei hiyo imefanyika nyakati za mchana katika ukumbi wa Kardinali Rugambwa, kando ya kanisa la Mtakatifu Petro-Oysterbay ikitanguliwa na Misa ya shukrani iliyofanyika katika Kanisa hilo asubuhi.
Jubilei hiyo imehudhuriwa na viongozi mbalimbali wakiwemo Rais Dk. John Magufuli na Mkewe Mama Janeth Magufuli, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan, Rais Mstaafu wa Awamu ya Nne Dk. Jakaya Kikwete, Rais Mstaafu wa Awamu ya Sita wa Zanzibar Dk. Amani Abeid Karume, Mjane wa Baba wa Taifa Mama Maria Nyerere, Mawaziri Wakuu Wastaafu Cleopa Msuya, Dk. Salim Ahmed Salim, Jaji Joseph Warioba na Edward Lowassa.
Misa Takatifu ya Shukrani imeongozwa na Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Arusha Mhashamu Askofu Josephat Lebulu na kuhudhuriwa na Maaskofu na Maaskofu Wakuu saba akiwemo Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo.
Akizungumza mwishoni Misa Takatifu, Rais Magufuli amempongeza Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa kwa kutimiza miaka 50 ya ndoa na ameeleza kuwa ndoa hiyo iliyowaunganisha wanandoa wanaotoka katika madhehebu tofauti ya Kikristo imetoa fundisho kubwa kuwa binadamu wanapaswa kuwa wamoja hata kama wana tofauti mbalimbali zikiwemo za kimadhehebu ya dini, siasa na kanda.
Rais Magufuli amesema miaka 50 ya ndoa ya Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa Katoliki na Mkewe Mama Anna Mkapa ambaye ni Muumini wa Kanisa la Kilutheri inawafundisha watanzania wote hususani wanasiasa kuishi kwa upendo na kuilinda amani waliyonayo na ametoa wito kwa viongozi dini kuendeleza juhudi zao za kuliombea taifa na kuwaunganisha wananchi licha ya tofauti walizo nazo.
Kwa upande wake Rais Mstaafu, Mkapa pamoja na kuwashukuru Viongozi wote, ndugu, jamaa na marafiki waliohudhuria Misa ya Shukrani na Jubilei hiyo ya miaka 50 ya ndoa yake amemshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuijaalia ndoa yake umri mrefu.
Rais Mstaafu Mkapa pia ametoa mwito kwa watanzania kupenda na kushirikiana huku akibainisha mafunzo aliyoyapata kutoka kwa viongozi wa dini kuwa "Kila mmoja ni zawadi kwa mwenzake"
Nae Askofu Mkuu wa Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo amempongeza Rais Mstaafu Mkapa na Mkewe Mama Anna Mkapa kwa kuadhimisha miaka 50 ya ndoa na amewasihi watanzania kuiga mfano mwema uliooneshwa na wana ndoa hao ambao wamedumu katika imani bila kuyumba.
Kardinali Pengo amesema ndoa ya Rais Mstaafu Mkapa anaifundisha jamii kuwa tunaweza kuishi kwa imani zetu bila kubadili dini
Rais Dkt John Pombe Magufuli akilakiwa na Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe wakati akiwasili kuhudhuria Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, wakati akiwasili kuhudhuria Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016. Lowassa alikuwa mshindani wake mkubwa katika kinyang'anyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015, ambapo Lowassa aligombea kupitia Chadema.
Rais Dk. John Magufuli akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, wakati akiwasili kuhudhuria Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016. Lowassa alikuwa mshindani wake mkubwa katika kinyang'anyiro cha Urais katika uchaguzi mkuu uliopita mwaka 2015, ambapo Lowassa aligombea kupitia Chadema.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri Mkuu wa zamani Edward Lowassa, wakati akiwasili kuhudhuria Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
"Maharusi" Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiingia kanisani tayari kwa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakiwa tayari kwa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa yao katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Paroko wa Parokia ya Mtakatifu Petro Fr. Stephano Kaombwe akiongoza Ibada ya ukumbusho wa ahadi za ndoa wakati wa Misa ya Jubilei ya Dhahabu (miaka 50) ya ndoa ya Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akimvisha pete Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa akivishwa pete na Mama Anna Mkapa katika kanisa la Mt. Petro jijini Dar es salaam leo Jumamosi Agosti 27, 2016
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mama Anna Mkapa
Mama Janeth Magufuli na Mama Maria Nyerere wakiwatakia amani Mzee Mkapa na Mama Anna Mkapa
Rais Dkt John Pombe Magufuli akimtakia amani Mhe. Edward Lowassa
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipokea hati malumu ya ndoa kutoka Vatican kwa Baba Mtakatifu Papa Francis kutoka kwa Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo
Rais Mstaafu Mhe Benjamin Mkapa na Mama Anna Mkapa wakipongezwa na Askofu Mkuu wa Kanisa Katoliki, Jimbo Kuu la Dar es Salaam, Mwadhama Polycarp Kardinali Pengo. PICHA ZAIDI>>BOFYA HAPA
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269