Baadhi ya watoto wanaotumikishwa kama wanajeshi kwenye maeneo ya vita
Shirika
la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF,limeonya juu ya ongezeko
la watoto wanaosajiliwa kujiunga na jeshi ili kupigana vita nchini
Sudani kusini.
Akiongea
baada ya kufanya ziara katika maeneo ya Bentiu na Juba nchini Sudan
Kusini, mkurugenzi mkuu wa UNICEF Justin Forsyth, alisema kuwa kuna hofu
kuwa huenda watoto zaidi wakaingizwa jeshini.
Pande zote tofauti zinatajwa kusajili wapiganaji watoto kwa mujibu wa Justin Forsyth,naibu mkurugenzi wa UNICEF.
Forsyth
amebainisha ongezeko la ushawishi wa watoto kujiunga na jeshi hususan
katika maeneo ya vijijini hali inayozua hofu ya kuenea zaidi kwa ghasia.
UNICEF
sasa ina hofu kuwa mzozo huo mpya huenda ukahatarisha maisha ya maelfu
ya watoto na kutaka shughuli hiyo ya kuwajiri watoto isitishwe mara
moja.
Takribani
watoto elfu kumi na sita wamesajiliwa katika makundi yanayoendesha
mapigano ikiwemo vikosi vya serikalitangu kuzuka kwa vita desemba 2013.RFI
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269