Rais Mstaafu Jakaya Kikwete akipokea Tuzo ya Uongozi wa Kisiasa na Utetezi kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Speak Up Afrika Bi Kate Campana, hafla iliyofanyika Alhamis jana , New York Marekani |
Shirika lisilo la Kiserikali la Speak Up for Afrika limemtunukia tuzo, Rais Mstaafu Jakaya Mrisho
Kikwete kutokana na uongozi wake wa kisiasa na utetezi wake kwa makundi ya jamii yaliyo katika mazingira magumu
hususani wanawake na watoto.
Utoaji wa Tuzo hiyo ya
uongozi wa kisiasa na utetezi , umekwenda sambamba na hafla ya
miaka mitano ya kuanzishwa kwa Taasisi ya Speak up Afrika. Hafla hiyo iliyofanyika jana Alhamisi Jijini New
York ilikuwa pia ni
sehemu ya kuhamasisha uchangiaji wa shughuli za
Taasisi hiyo.
Mchango ambao umetambuliwa na Speak Up Afrika,
taasisi ambayo imekuwa ikifanya kazi
kwa Karibu na Rais Mstaafu Kikwete, ni katika maeneo ya upelekaji na usambazaji wa huduma za msingi
za afya hususani afya ya mama na mtoto,
udhibiti wa ugonjwa wa malaria kupitia kampeni ya malaria haikubaliki ,usambazaji wa
vyandarua vyenye viatilifu, kampeni
ya lishe bora, na kampeni ya
chanjo kwa watoto.
Pamoja na
kutambua juhudi za Rais Mstaafu
Kikwete katika kuyasemea maeneo
hayo, Taasisi hiyo kupitia Mkurugenzi wake Mtendaji Bi. Kate Campana pia imemtambua kama kiongozi ambaye amekuwa mstari wa mbele wa kulisema Bara la Afrika kila mara alipopata fursa
ya kufanya hivyo wakati akiwa
madarakani na hata baada ya kustaafu.
Rais kikwete ameelezwa katika hafla
hiyo iliyowashirikisha wadau wa kada
mbalimbali, kama kiongozi wa kisiasa ambaye amezigusa nyoyo za watu wengi
kujitolea kwaajili ya watu wenye mahitajio ya kupata huduma za msingi za
kijamii ambazo au wameshindwa kuzipata
kutokana na kipato kidogo au haziwafikii kabisa.
Akipokea Tuzo hiyo, Rais Mstaafu Kikwete , amesema Tuzo hiyo ni ya
watoto wote waafrika ambao ndio waliomfanya asimame mbele
ya wageni waalikwa.
“ Ni kwa sababu yenu ndio sababu
nimetenga muda wangu baada ya kustaafu
kusukuma mbele agenda ya kuboresha
maisha yanu. Ninafanya hivyo kwasababu makuzi yangu yalikuwa kama ya mtoto yeyote yule wa kiafrika, nimeyaishi maisha wanayo ishi. Na kwa hiyo ninaelewa fika hamu na kiu yao ya kuwa na maisha bora na afya njema”. Akasema
Kikwete na kushangiliwa na wageni waalikwa.
Akaongeza kuwa ,
mafaniko ambayo ameyapata katika
juhudi hizo za kufikisha huduma
za msingi za kijamii kwa makundi yenye mahitaji yametokana na mambo mawili makubwa moja
ni aina ya uongozi alioutumia kusukuma harakati hizo. Na pili uhamasishaji uliofanyika katika kupiga vita malaria kupitia Speak Up Afrika na
kampeni yao ya malaria haikubaliki.
“ Nisingeweza kuyafanya
niliyoyafanya bila uungugwaji mkono
na ushirikiano wa karibu nilioupata na ninaoupata kutoka taasisi za kimataifa ikiwamo hii ya
Speak Up Afrika. Ndio maana kwa mfano,
tumeweza kupunguza visa vya malaria kwa
theluthi mbilli,
tumefanikisha upatikanaji wa
chanjo kwa asilimia 96 kwa watoto wote na kupunguza vifo vitokanavyo na malaria kwa
nusu.” Akaeleza Kikwete na
kushangiliwa tena.
Akasema, anamini katika ushirikiano
na wadau mbalimbali kama akina Ray
Chambers kupitia kampeni ya hakuna tena
malaria, Taasisi ya Bili na Melinda
Gates na Gavi Vaccination Alliance
ambayo anashirikiano nayo kwa karibu
katika kampeni ya chanjo kwa wote.
Rais
Mstaafu amewahakikishia watendaji
wa Speak Up Afrika kwamba ataendelea kufanya kazi nao kwa karibu kutokana
kile alichosema amejionea mwenye kazi nzuri wanayoifana.
Akawasihi
wadau mbalimbali kuichangia
taasisi hiyo kwa kile alichosema,
inafanya kazi kubwa ya siyo tu kufikisha
huduma za kijamii pale zinapotakiwa lakini
pia imekuwa ni kipaza sauti cha Afrika.
Wengine waliopewa Tuzo kwa kutambua
michango yao kwa jamii ni pamoja na Professa Awa Marie Coll- Seck, Waziri wa
Afya wa Senegal, Bibi Toyin Saraki,
mwanzilishi wa Taasisi ya
Wellbeing Afrika ambayo pia imekuwa ikitoa elimu na misaada kwa wanawake na watoto
pamoja na elimu kwa wakunga na kutambua
kazi nzuri, kubwa na ngumu ya
kuwahudumia wanawake wenzao wanapojifungua.
Na Bwana Kabirou Mbodje ambaye ni
Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Wari.
Taasisi ya Speak
Up Afrika imeanzishwa
na wanawake na inaongozwa na wanawake. Ni taasisi ambayo imejijengea
uweo na sifa kubwa ndani ya kipindi cha
miaka mitano tangu kuanzishwa
kwake.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269