Mtangazaji wa TV ya Korea akitangaza habari za jaribio hilo
Shirika
la habari la serikali ya Korea Kaskazini limesema taifa hilo limefanya
majaribio ya bomu kupima uwezo wa bomu lake la nyuklia la kurushwa kwa
kombora hatua ambayo imeshutumiwa vikali na jamii ya kimataifa.
Mlipuko wa bomu hilo umesababisha tetemeko la ardhi katika eneo lililofanyiwa majaribio.
Tetemeko hilo lilikuwa na nguvu ya 5.3 kwenye vipimo vya Richter.
Maafisa
wa jeshi la Korea Kusini wanakadiria kwamba mlipuko huo ulikuwa sawa na
wa kilo tani kumi za TNT, ukubwa sawa na wa bomu lililoangushwa
Hiroshima na Marekani wakati wa vita vikuu vya pili vya dunia. Baadhi
wanasema huenda bomu hilo la Korea Kaskazini likawa lilikuwa na nguvu ya
kilo tani 20.
Bomu lililoangushwa Hiroshima mwaka 1945 lilikuwa na nguvu ya kilo tani 15 (tani 15,000).
Bomu
lenye nguvu zaidi la nyuklia lililowahi kulipuliwa lilikuwa lile
lililopewa jina Tsar-bomba, ambalo lililipuliwa na Urusi mwaka 1961.
Korea Kaskazini imesea jaribio hilo limefanikiwa
Lilikuwa na nguvu ya mega tani 50, sawa na nguvu ya tani milioni 50 za TNT (50,000,000).
Wataalamu
bado wanaendelea kudadisi iwapo lilikuwa bomu la haidrojeni, jambo
ambalo linaweza kulipa nguvu zaidi kushinda mlipuko wa bomu la kawaida
la nyuklia.
Korea Kaskazini yarusha makombora tenaUN yatishia kuichukulia hatua Korea Kaskazini
Mwanamke maarufu zaidi Korea Kaskazini
Hilo likithibitishwa, basi itakuwa ni mara ya tano kwa Pyongyang kutekeleza jaribio la silaha za kinyuklia.
Jaribio la leo limetekelezwa siku ambayo serikali inaadhimisha kuanzishwa kwa taifa la sasa la Korea Kaskazini mwaka 1948.
Jamii ya kimataifa imeghadhabishwa na hatua hiyo ya Korea Kaskazini.
Rais Kim Jong-un ameonyeshwa kwenye runinga akiwa amejaa tabasamu
Rais wa
Korea Kusini Park Geun-hye ametaja jaribio hilo kuwa "jaribio la
kujiangamiza" ambalo linaonyesha "kutomakinika" kwa kiongozi wa Korea
Kaskazini Kim Jong-un.
Bi Park,
ambaye amesitisha ghafla ziara yake ng'ambo, amesema baada ya kutekeleza
jaribio hilo la tano la nyuklia "serikali ya Kim Jong-un itakaribisha
vikwazo zaidi na kutengwa zaidi na jamii ya kimataifa."
Korea Kaskazini yafanya 'jaribio kubwa la nyuklia'
"Uchokozi kama huu utaongeza kazi safari yake ya kuelekea kwenye maangamizi."
Bi Park alifanya pia amzungumzo ya dharura na Rais wa Marekani Barack Obama kwa njia ya simu.
Kuvumiliwa
China,
mshirika mkuu wa Korea Kaskazini kidiplomasia, pia imeshutumu hatua hiyo
na kuihimiza Pyongyang kukoma kuchukua hatua ambazo zinaweza kuzidisha
hali.
Waziri mkuu wa Japan Shinzo Abe, amesema majaribio kama hayo ya Korea Kaskazini hayawezi kuvumiliwa.
Bw Shinzo Abe. Japan imeilalamikia Korea Kaskazini
Lakini
mwandishi wa BBC anayeangazia Korea anasema wapinzani wa Pyongyang
wanatatizika kuhusu ni hatua gani wanafaa kuuchukulia utawala wa Korea
Kaskazini.
Tayari waliwekea taifa hilo vikwazo Januari baada ya Pyongyang kufanya jaribio la nne ya nyuklia. BBC
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269