Profesa
Mark Mwandosya (kushoto) akielezea uzoefu wake alipokuwa Kamishna wa
Kwanza wa Nishati na Maendeleo ya Petroli, Wizara ya Nishati na Madini
mwaka 1985 mara alipomtembelea Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na
Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo ofisini kwake
jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Juliana Pallangyo. Kulia ni
mwakilishi kutoka Kampuni ya Pan African Energy aliyeambatana na Profesa
Mark Mwandosya, Jacqueline Kawishe.
Naibu
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati
Dkt. Juliana Pallangyo akielezea maendeleo ya Idara ya Nishati katika
kikao hicho.
Kutoka
kushoto, Kaimu Kamishna wa Nishati na Maendeleo ya Petroli Nchini
kutoka Wizara ya Nishati na Madini, James Andilile, Naibu Katibu Mkuu
wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati Dkt. Juliana
Pallangyo, Profesa Mark Mwandosya na mwakilishi kutoka katika kampuni ya
Pan African Energy, Jacqueline Kawishe wakiwa katika picha ya pamoja.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269