NA
K-VIS BLOG/MASHIRIKA YA HABARI
WAGOMBEA
wa kiti cha Rais nchini Marekani, Bibi.Hilalary Clinton, wa Chama Cha Democrat,
na Bw. Donald Trump wa Chama Cha Republican, “wameparurana” wakati wa mdahalo
wa kwanza uliofanyika alfajiri ya leo Septemba 27, 2016 kwenye ukumbi wa Chuo Kikuu cha Hofstra jijini
New York nchini Marekani.
Katika
mdahalo huo wa kwanza ulioongozwa na Lester Holt na uliokuwa
live kupitia runinga za nchi hiyo, wagombea hao walitakiwa kujikita kwenye
masuala ya Sera ya ya Nje ya Marekani, Usalama wa Taifa hilo kubwa klabisa
Duniani, Uchumi, Nishati na Mazingira, Ajira, Ubaguzi na Ugaidi
Wakati
Trump, alijinadi kuwa yeye ndiye anayefaa kuliongoza taifa hilo kwa vile
anakuja na mkakati mpya wa kulirudishia heshima ya “kimabavu” ya taifa hilo
kwani mpinzani wake hawezi kuleta mabadiliko yoyote kwani kwa miaka 30 ya uwepo
wa bibi Clinton kwenye anga za kiutawala, hakuweza kufanya lolote.
Naye
Bibi Ckinton kwa kejeli alielezea matamshi makali na yenye utata ya Donald Trump,
yanaonyesha anavyoishi kwenye uhalisia wa hulka yake, “Donald you live on your
reality”.
Hivi
ndivyo Donald Trump alivyo “mnanga” Bibi Clinton, walipotakiwa kuelezea
mikakati yao katika Sera za Nje na Usalama wa taifa.
“Bibi
Clinton, umekuwa ukipambana na wanamgambo wa Kiislamu wa ISIS kwa karibu maisha
yako yote ya utu uzima”, Trump alisema.
Naye
Bibi Clinton kuhusu suala hilo aliilaumu Russia kwa kuanzisha vita mpya ya
kimtandao dhidi ya Marekani na kusema, “Russia na Rais Vladimir V. Putin
wameanzisha vita mpya ya kutumia mitandao kwa kufanya udukuzi, wa taarifa nyeti
za kibinafsi na za taifa hilo la Marekani kwenye mtandao wa Internet na kwamba,
yeye akiwa Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Marekani atahakikisha Russia, China, au
kikundi chochote chenye nia mbaya na Marekani, kinadhibitiwa kwa kuimarisha
intelijensia na kushirikiana na makampuni yanayoendesha mitandao nchini humo.
Kuhusu
suala hilo hilo la Sera ya Nje na Usalama, Donald Trump alisema, “Islamic State(ISIS)
wasingeweza kutetemesha ulimwengu kama Marekani ingesalia Iraq, “kuondoka kwa
Marekani nchini humo kumeacha mwanya unaowafanya sasa ISIS kufanya watakalo na
kutapakaa kote Iraq na Syria, Marekani ilipaswa kuchukua mafuta yote ya Iraq
kwani mafuta hayo ndiyo wanayotumia ISIS kujipatia kipato na kuendesha vita na
kufadhili washirika wao nje ya Iraq.” Alisema Trump
Trump
aliweka msimamo wake kuwa Jumuiya ya NATO haina faida na Marekani, kwani
asilimia 70 ya michngo yote ya kuendesha NATO imekuwa ikitolewa na Marekani, na
kwamba, washirika wa NATO wameshindwa kuisaidia Marekani kupambana na Ugaidi na
badala yake wanafanya mambo yasiyokuwa na faida na Marekani na kwamba yeye
akiwa Rais, ni lazima kila taifa litoe mchango sawa vinginevyo Marekani haiwezi
kuendelea kuzilinda nchi za NATO bure bure tu, la sivyo watalazimika kulipia
gharama.
Hata
hivyo Bibi Clintoa alimfahamisha mpinzani wake kuwa Kama ilivyo msimamo wa
kisera wa Marekani, aliyeandaa na kusaini makubaliano ya kuyaondosha majeshi ya
Marekani nchini Iraq, ni Rais George Bush, na siyo Barack Obama, alichofanya
Obama ni kutekeleza maamuzi ya kisera yaliyofanywa na mtangulizi wake kwa niaba
ya Marekani, na kuhusu NATO Bibi Clinton alieleza umuhimu wa ushirika huo
katika usalama wa Marekani, kwani kila Marekani inaposhiriki vita sehemu fulani
ya Dunia, wamekuwa wakishirikiana na wenzao wa NATO katika noperesheni
mbalimbali za kijeshi ikiwemo kubadilishana taarifa za kiintelijensia kuhusu
mapambano dhidi ya ugaidi.
Mdahalo
wa pili unatarajiwa kufanyika Oktoba 10 na watatu na wa mwisho utafanyika
Oktoba 20. Uchaguzi wa Marekani unatarajiwa kufanyika Novemba mwaka huu.
Muongoza mdahalo, Lester Holt |
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269