Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda (kushoto) akizungumza na Wananchi walio fika katika viwanja vya
Mnazi Mmoja kupata vipimo na kupatiwa ushauri na Madaktari kutoka
Hospitali Mbalimbali Jijini Dar es Salaam
Wananchi wakiwa na watoto wao katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Wananchi wakiwa katika mistari ambao hawajapata namba
Mkuu wa Idara ya magonjwa ya Dharura na
Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma Mfinanga (kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa Zoezi la kupima vipimo
kwa wananchi bure lililo ratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam Paul Makonda kwa kushirikiana na Madaktari kutoka Hospitali
mbalimbali za Dar es Salaam ikiwemo, Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aga
Khan Hospital, Taasisi ya Moyo ya Jakaya Kikwete ikiongonzwa na Rais wa
Chama cha Madaktari Figo Tanzania na pia ni Daktari Bingwa wa Figo Dk.
Onesmo Kisanga
Mganga Mkuu wa Mkoa
wa Dar es Salaam, Grece (kushoto) Magembe akiwaonyesha jambo wananchi
walio jitokeza kupata huduma ya vipimo kutoka kwa Madaktari wa
Hospitali mbalimbali ikiwemo Hospitali ya Taifa Muhimbili mkoa wa Dar es
Salaam ilioratibiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda lililofanyika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Jijini humo na
kutokana na mwitikio wa wananchi huwenda ziku zitaongezwa baada ya Mkuu
huyo kujadiliana na madaktari hao ambapo Septemba 25 hapo awali ilikuwa
ndio siku ya kuhitimisha zoezi hilo
Wafanyakazi katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam wakiwa katika picha ya pamoja
Zuhura Shaba (54) akiwa amebebwa na
baadhi ya Madaktari na wafanyakazi wa Afya baada ya kujikuta amepoteza
fahamu mara baada ya kufika katika viwanja vya Mnazi Mmoja Dar es Salaam
, baada ya muda na mpiga picha hizi alibahatika kuongea nae na kuanza
kusema kwa utaratibu kinacho msumbua na kueleza mengi baada ya
kumdadisi alisema, yeye ni Mtoto wa 7 na baba yake ezi za uhai wake
miaka ya nyuma aliwahi shika nyadhifa mbalimbali Serikalini kama,
Waziri wa Afya, Meneja Mkonge Tanga, aliwahi kuwa Mbunge, hivyo
anamshukuru Mkuu wa Mkoa na Mungu amuongoze kwa kila anachokifanya kwa
Jamii ya Kitanzania na kumshukuru Rais wa Tanzania kwa kumpa maona ya
kumchagua kijana huyu, Makonda kuwa Mkuu wa Mkoa na kuishukuru timu
nzima ya Madaktari kwa moyo wao kuona jamii ya kitanzani bado inahali
duni na kushirikiana na Mkuu wa Mkoa kutuletea zoezi hili, nashukuru
baada ya kujikuta napoteza fahamu nimejikuta nipo katika chumba huduma
ya haraka na kupata huduma na sasa najiona ninanafuu.
Mkuu wa Wilaya ya
Ilala Bi Sophia Mjema (kushoto) akishiriki zoezi la kugawa namba kwa
wananchi walioitikia wito wa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam
Baadhi ya Wananchi wakiwa wamenyoosha mikono wakitarajia kupata namba kwa ajili ya kupatiwa huduma ya vipimo
Askari Polisi akizungumza na baadhi ya Wananchi waliojitokeza katika viwanja vya Mnazi Mmoja
Joice Mgeta akipatiwa vipimo na Dk.
Danieli Chacha (kushoto) mara baada kujikuta anaishiwa nguvu ghafla
akiwa katika foleni ya kusubiri kupata namba , kulia ni Mkuu wa Idara
ya magonjwa ya Dharura na Ajali Hospitali ya Taifa Muhimbili Dk. Juma
Mfinanga
(PICHA ZOTE NA KHAMISI MUSSA)
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269