Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao (kushoto)
akimkambidhi mmojawapo wa washindi wa mashindano ya sauti, Hilda
Malecela mfano wa runinga ya kisasa yenye ukubwa wa inchi 40 kutoka
kampuni hiyo. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia
fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes
yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmojawapo
wa washindi wa sindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela
akikumbatiana na majaji baada ya shindano ilo kuisha, akishuhudia tukio
hilo kushoto ni Afisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao
na kulia ni majaji na washindi wengine. Washindi 10 walipatikana katika
shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za
makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
washindi
10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa
kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada
ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano
hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao
makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Washindi
10 wa shindano la vipaji vya sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa
kushirikiana na ubalozi wa China Tanzania wakiwa mbele ya jukwaa baada
ya kutangazwa washindi. Washindi hao 10 walipatikana katika shindano
hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao
makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing, China.
Ofisa
Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang Liao akifanya mahojiano na
waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa shindano la vipaji vya
sauti lililoandaliwa na StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa China
Tanzania. Washindi 10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia
fursa ya kwenda kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes
yaliyopo jijini Beijing, China.
Mmoja
wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Hilda Malecela akionyesha
uwezo wake wa kuigiza sauti mbele ya majaji jukwaani. Washindi 10
walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda kufanya
kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini Beijing,
China.
Mmoja
wa washiriki wa shindano la vipaji vya sauti, Rukia Hamdani akiwa mbele
ya majaji jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi
10 walipatikana katika shindano hilo na kujipatia fursa ya kwenda
kufanya kazi katika ofisi za makao makuu ya StarTimes yaliyopo jijini
Beijing, China.
Mshiriki
wa shindano la vipaji vya sauti, Coletha Raymond akiwa mbele ya majaji
jukwaani baada ya kuonyesha uwezo wake wa kuigiza. Washindi 10
walipatikana katika shindano.
Na Dotto Mwaibale
Hatimaye
shindano la kusaka vipaji vya sauti lililoandaliwa na kampuni ya
StarTimes kwa kushirikiana na ubalozi wa Chini nchini Tanzania
limemalizika mwishoni mwa wiki hii kwa watanzania 10 kujipatia fursa ya
kwenda kufanya kazi katika makao makuu yake yaliyopo jijini Beijing.
Akizungumza
baada ya shindano hilo Dar es Salaam juzi , Hilda Malecela kutoka Dar
es Salaam ambaye ndiye aliyeongoza kwa kupata alama nyingi kutoka kwa
majaji alisema kuwa anashukuru sana kupata fursa hiyo ya kuonyesha kila
kipaji alichonacho kwani haikuwa kazi rahisi.
‘’Kwanza
kabisa nashukuru kwa ushindi huu, haikuwa kazi rahisi kwani ushindani
ulikuwa ni mkubwa ukizingatia washiriki walioingia hatua ya fainali wote
walikuwa wana uwezo mkubwa sana. Nawashukuru majaji kwa kunipa moyo
tangu awali na hatimaye kuniamini kwamba nina kitu ambacho ninaweza
kukitoa kwa watanzania kupitia kipaji change cha sauti. Fursa
niliyoipata mimi pamoja na washindi wenzangu tisa ni jambo la kujivunia
na kuitumia ipasavyo.’’ alisema . Malecela
‘’Napenda
kuwaahidi watanzania kuwa nitaitumia nafasi hii vema kuhakikisha
nafanya kazi nzuri ili wao waendelea kuburudika na kujifunza zaidi
kupitia filamu na tamthiliya. Nawapongeza pia StarTimes kwa kutambua
umuhimu wa Kiswahili na kuja ubunifu huu ambao haujawahi kutokea nchini.
Mara nyingi tumekuwa tukiona mashindano ya kuimba, kuigiza na kucheza
lakini si kwa upande wa sauti. Wamepiga hatua kubwa sana kwa kweli
ambayo inastahili kuigwa na makampuni mengine.’’ alimalizia mshindi huyo
aliyeongoza kwa kuwa na alama nyingi zaidi kutoka kwa majaji
Naye
kwa upande wake Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTimes Tanzania, Lanfang
Liao amebainisha kuwa amefurahi kuona shindano la kusaka vipaji vya
sauti limepokewa kwa muitikio mkubwa na watanzania sehemu mbalimbali za
nchi.
‘’Hatukutegemea
kama watanzania wengi wangevutiwa na shindano hili lakini imekuwa ni
kinyume chake kwani imedhihirika kuwa wapo wasanii wengi sana wenye
vipaji vya sauti. Sanaa ina uwanja mpana sana ni namna tu msanii
mwenyewe anavyoamua anakitumia vipi kipaji alichonacho. StarTimes
tumebaini kutoka kwa wateja wetu kuwa filamu na tamthiliya
zilizotafsiriwa na kuingiziwa sauti kwa lugha ya Kiswahili zinapendwa
sana. Hivyo tukaona ni vema kuviibua vipaji ili tufanye nao kazi hiyo
kwa manufaa ya watanzania.’’ alisema Liao
‘’Tunaamini
kupitia shindano hili tumeweza kutoa ajira kwa watanzania 10
watakaokwenda kujumuika na wenzetu waliopo makao makuu jijini Beijing,
China katika kuzalisha kazi zilizo bora kabisa. Nawasihi washindi
waliopata fursa hii kuitumia vema kwa kufanya kazi kwa bidii kwani
ninaamini wanastahili mpaka kuchaguliwa na majaji kuwa vinara dhidi ya
wenzao 18 waliofikia hatua ya fainali. StarTimes tunaahidi kuendelea na
zoezi hili wakati ujao kwani bado uhitaji ni mkubwa na sisi siku zote
tupo kwa ajili ya kuwapatia kile wateja wetu wanachokitaka.’’
alihitimisha Ofisa Mtendaji Mkuu wa StarTime nchini
Katika
fainali hizo washindi wa kwanza, pili na watatu; Hilda Malecela -
kutoka DSM, Safiya Ahmed kutoka Zanzibar na Sadiq Kututwa - kutoka
Zanzibar) walizadiwa runinga za kisasa zenye ukubwa wa inchi 40, 32 na
24 kila mmoja na StarTimes kutokana na kuongoza kwa alama nyingi katika
fainali hizo huku washindi saba wakipatiwa simu za mkononi za kisasa
kutoka StarTimes.
Kwa
ujumla washindi kumi waliopatikana ni; Hilda Malecela(DSM), Safiya
Ahmed(ZNZ), Sadiq Kututwa(ZNZ), Mathew Philip Mgeni(Arusha), Maisala
Abdul(DSM), Rukia Hamdan(ZNZ), Richard Rusasa(DSM), Happiness Stanslaus -
Nyamayao(DSM), Jamila Hassan(DSM) na Abraham Richard(DSM). Na wote
watapata fursa ya kwenda kufanya kazi katika makao makuu ya StarTimes
yaliyopo jijini Beijing, China kwa mkataba wa muda wa mwaka mmoja.
Katika
mashindano hayo takribani washiriki zaidi ya 547 walijitokeza katika
usaili uliofanyika katika mikoa ya Arusha (Agosti 27), Zanzibar
(Septemba 3) na Dar es Salaam (Septemba 10) na hatimaye washiriki 18 tu
wakabakia na kutinga hatua ya fainali.
Washiriki
18 waliotinga hatua ya fainali ni kama ifuatavyo: kwa mkoa wa Arusha ni
Mathew Philip Mgeni, Dorcas Francis, Halima Hussein, Janeth N Molely na
Hilda Kinabo; Zanzibar ni Safiya Ahmed Said, Sadiq Kututwa Abdalahh,
Rukia Hamdan, Imatu Obeid Fabian na Mohamed Said Mohamed; na Dar es
Salaam ni Hilda Malecela, Abraham Richard, Happiness Stanslaus
‘Nyamayao’, Richard Rusasa, Emanuel Landey, Coletha Raymond, Jamila
Hassan na Maisala Abdul.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269