Raia wasiopungua 18 wameuliwa katika eneo la
makaazi ya raia la mji wa Mosul kaskazini mwa Iraq katika shambulio
lililofanywa na muungano unaoongozwa na Marekai kwa kisingizio cha
kupambana na ugaidi nchini humo.
Duru moja ya Iraq imetangaza kuwa watu 18 wakiwemo wanawake 14
wameuawa katika shambulio la ndege za kivita za muungano unaoongozwa na
Marekani katika eneo la al-Ba'ath mjini Mosul makao makuu ya mkoa wa
Neinawa.
Mauaji ya wanafunzi mjini Mosul na shambulio dhidi ya hafla ya
maombolezo katika eneo la Daquq, mjini Kirkuk lililosababisha kuuawa
raia 25 wakiwemo wanawake 15 ni miongoni mwa hujuma za karibuni
zilizofanywa na muungano unaoongozwa na Marekani nchini Iraq na
kunyamaziwa kimya na Umoja wa Mataifa.
Maafisa wa jeshi la Marekani wanadai kuwa huwalenga raia wa
Iraq kimakosa, madai ambayo hayawezi kutetewa kwa kuzingatia ramani
zilizopo za operesheni za kuukomboa mji wa Mosul kutoka kwenye makucha
ya kundi la kigaidi na kitakfiiri la Daesh na kujulikana wazi ngome za
kundi hilo la kigaidi.
Mnamo mwezi Septemba mwaka 2014, muungano eti wa kupambana na Daesh
unaoongozwa na Marekani ulianzisha mashambulio ya anga ndani ya ardhi za
Syria na Iraq kwa kisingizio cha kupambana na kundi hilo la kigaidi na
kitakfiri.../
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269