Breaking News

Your Ad Spot

Nov 28, 2016

WAZIRI LUKUVI SITAKI KULILIWA ,TATUENI WENYEWE KIGOMA

 NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA WAZIRI wa Ardhi,Maendeleo ya Nyumba na Makazi Williamu Lukuvi ameagiza mikoa yote Nchini wakome kuililia wizara hiyo katika kutatua sintofahamu ya migogoro ya ardhi ,badala yake halmashauri zake ziwajibike kuondoa kero hiyo kwa wananchi,kwa kuwa ndio chanzo cha changamoto hiyo. Akitoa kauli hiyo mkoani kigoma jana katika ziara ya siku tatu inayolenga kusikiliza kero na malalamiko mbalimbali yanayohusiana na ardhi kwa nia ya kutoa maelekezo sahihi juu ya kero hiyo inayoikabili taifa kwa ujumla,ambapo chimbuko kubwa ni wanasiasa wakishirikiana na watumishi wa umma katika kugawa vijiji,vitongoji ili waendelee kushika nyadhifa za ubunge na udiwani. Lukuvi alifafanua kuwa, changamoto kubwa inayoikabili taifa kwa kasi ni ardhi ambapo watendaji,wenyeviti , wataalamu na wanasiasa hasa wabunge na madiwani ambao wanashaka ya kutochaguliwa na vijiji ima kitongoji Fulani ambacho kina wapigakura wengi huandaa mpango wa kijiji hicho kugawanywa mara mbili bila kushirikisha wananchi husika. Alisema kwa kitendo cha kuvigawa vijiji kila wakati wa uchaguzi ni kero ya migogoro ya ardhi,ambapo kila wilaya kupitia mkoa wake ndio chanzo cha kuwepo kwa kero hiyo kutokana na usimamizi mbovu wa sheria na taratibu husika bila kujali athari ya ugawaji wa vijiji bila kushirikisha wananchi wakazi wa eneo husika hatimaye umwagaji wa damu wa wanyonge unalitafuna taifa . “najua kuna baadhi ya wabunge wanaleta kilio cha kutaka vijiji Fulani vigawanywe baada ya kutathimini watashindwa kwenye uchaguzi ,mawazo ya wachache italigharimu taifa, ifikapo Desemba 30,mwaka huu mikoa ikamilishe kutembelea maeneno yenye migogoro ya ardhi na wapange mikakati thabiti ya kutatua kero hiyo na mabaraza ya ardhi yatimize wajibu wake” alifafanua waziri huyo. Akiri awali kulikuwa na uchoraji na utoaji wa ramani usio na uhalisia wa eneo husika kwa kuwa wachoraji wapo jijini Dar es salaam na kuwataka idara husika wapeleke mapendekezo yaliyo sahihi baada ya kupitia taratibu zote za vijiji husika kwa kushirikisha jamiii ili kuepuka migongano ya maslai ndani ya jamii lengwa. Awali Mwenyekiti wa wakulima katika kijiji cha Mtanga wilayani kasulu Kidenya Munyelesingo alitoa malalamiko kwa kiongozi huyo,kuwa zaidi ya hekari 800 za kijiji hicho zimeporwa na wakubwa wa wilaya hiyo kwa kujigawia kila mmoja hekari 100 na wengine 200 kinyume cha utaratibu huku wananchi wakikosa meneno ya kilimo. Mwisho.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages