MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma Kanali Marco Gaguti (katikati) akifafanua jambo mbele ya Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia,
pamoja na kamati ya Ulinzi na Usalama ya Tanzania na Burundi katika
kujadiliana sakata la Wahamiaji wengi wengi kuanza kuingia nchini
Tanzania kwa kasi tangu Januari,2017.
MKUU wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti (kushoto) akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba nchini Burundi,(Musitanteri) Niyonkuru Laetitia
Mkuu wa Wilaya Ya Buhigwe akisalimiana Na Wanajeshi wa Burundi mpakani mwa Tanzania na Burundi
Mkuu wa Wilaya ya Buhigwe wa pili kulia akiongozana na kamati ya ulinzi na usalama kuingia mpakani mwa Burundi na Tanzania
Na Rhoda Ezekiel Kigoma.
MKUU
wa wilaya ya Buhigwe mkoa wa Kigoma kanali Marco Gaguti amewaonya
wakimbizi wenye historia ya uhalifu nchini Burundi wanaoingia Nchini
Tanzania, kwa kigezo cha kuomba hifadhi ya ukimbizi kwa kuhofia
wasikamatwe kwa uhalifu walioufanya Nchini mwao, kuwa ikibainika hatua
kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha, Gaguti aliuomba
uongozi wa Nchi ya Burundi kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na
usalama vya Wilaya hiyo iliyopo Mpakani, kuwabaini waomba hifadhi hao
wanaoingia Nchini kwa kukimbia uhalifu walioufanya Nchini mwao na kuja
kuendeleza vitendo hivyo wanapo ingia Nchini.
Hayo yalibainika
jana wakati wa Kikao cha majadiliano baina ya Mkuu huyo na Mkuu wa
Wilaya ya Mabanda Mkoa wa Makamba Nchini Burundi, alipokuwa akihoji ni
kwanini wahamiaji wengi wanaongezeka Nchini wakidai wanakimbia vurugu
zinazo endelea Nchini mwao ambapo kwa Mwezi january waliingia waomba
hifadhi 2230, ambapo ilibainika wengi wao wanadai wanakimbia kukamatwa
kwa kujihusisha na uhalifu na wengine kukimbia njaa iliyopo majumbani
kwao.
Gaguti alisema kumekuwa na ongezeko kubwa la wahamiaji
wanaoingia Nchini wakidai kukimbia vitisho wanavyo pewa na kikundi cha
Vijana wa chama tawala kinacho julikana kama ( IMBONELAKULE), ambapo
wanakuja kuomba hifadhi katika Nchi ya Tanzania ilihali Nchi yao ina
amani ya kutosha na wengine kukimbilia kambini kupata huduma za bure
kwa kuhofia njaa nchini mwao .
Hali
iliyopelekea Waziri wa Mambo ya ndani kusitisha zoezi la Waomba hifadhi
kuingia Nchini kwa kigezo cha kukimbia njaa Nchini mwao na kukimbilia
Tanzania ili waweze kupata Msaada wa chakula , ni lazima Afanyiwe
mahojiano na atoe sababu zilizo mfanya akimbie iliaweze kupatiwa kibali
cha kuwa mkimbizi.
Hata hivyo Kanali Gaguti aliwaomba viongozi
hao kutoa ushirikiano kwa vyombo vya ulinzi na usalama kuwabaini
wahalifu hao waweze kurudishwa Nchini mwao kuepukana na vitendo vinavyo
endelea na ongezeko la waomba hifadhi kuingia Nchini bila kufuata
utaratibu.
'' leo nilikuwa natembelea vituo na kuona ongezeko la
wahamiaji lakini serikali imetoa maelekezo mapya ikiwemo kuwatambua na
kujua sababu za kukimbia Nchini mwao, lakini kama atakuwa na sababu za
Msingi hata pata fursa ya kuwa mkimbizi, lakini pia nikuombe ushirikiano
kama kuna taarifa za watu ambao ni wahalifu upewe taarifa mapema kabla
ya mambo kubadilika ili tuweze kuchukua tahadhari mapema kwa pande zote
mbili" alisema kanali Gaguti.
Naye mkuu wa Wilaya ya Mabanda Mkoa
wa Makamba (Musitanteri)Niyonkuru Laetitia alisema kwa sasa nchi ya
Burundi ni tulivu na wanaokimbia nchini mwao ni wale wanaokimbia njaa
na wengine kukimbia uhalifu aliofanya nchini Burundi na kuja Tanzania
kuomba hifadhi.
Alisema wengi waliofika Tanzania ni wale
waliokimbia kwa mambo yao binafsi na wengine ni wale wakimbizi
waliorudishwa BUrundi kipindi cha nyuma wanaokimbia wengi wanakuja kwa
kigezo cha kupelekwa nje ya Nchi kama vile America na Ulayana Nchi
nyingine ilikuwafuata ndugu zao walio pelekwa huko .
Aidha
aliuomba Uongozi wa Tanzania kabla ya kuwapokea wahamiahi hao kuchukua
vitambulisho vyao ilikubaini walio kimbia tuhuma zinazo wakabili, pia
kumekuwa na tetesi wengi wao wanaoingia kuomba hifadhi wanakuja
makambini kujifunza namna wanavyo weza kwenda kuipindua Nchi kwa
kupigana pindi wanapo wabaini waweze kuwakabidhi kwa Serikali ya
Burundi.
Kwa upande wao baadhi ya Waomba hifadhi waliofika katika
maeneo ya kupokelea waomba hifadhi hao kwa mahojiano waweze kuingia
kambini ,wengi wao walidai wanakimbia vikundi vya IMBONELAKULE vinavyo
wafuata Nyumbani kwao usiku na kuwapiga na kuwatishia usalama wao hali
inayo walazimu kukimbilia Tanzania , suala lililo kanushwa na Mkuu wa
Wilaya ya Mabanda.
Nizigimana Silivesta ni moja kati ya waomba
hifadhi kutoka Burundi, alisema kinacho wapelekea kukimbia Nchini mwao
ni hali ya kiusalama kuwa ndogo kumekuwa na tabia ya vikundi vya watu
vinavyo wafuata kuwatisha kutokana na baadhi ya ndugu zao walio kimbilia
nchini kuwa wanamahusiano nao na wanaipinga serikali.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269