Baadhi ya wafanyakazi wakizungumzia hali ilivyokuwa juu ya kuwepo kwa taarifa ya kupigwa kwa wenzao mgodini hapo.
Eneo la mgodi Kazi zikiendelea .
Baadhi ya mawe ambayo yamekuwa yakitoa dhahabu yakiwa yamekusanywa sehemu moja
Wafanyakazi wa kampuni ya RZ wakijiandaa kuingia kwenye mashimo kwaajili ya utoaji wa mawe ya dhahabu.
Meneja wa
Mgodi huo,Guixue Liu (kulia),akiwa na Mwanasheria wa Mgodi Huo Frances Kiganga
wakiangalia namna kazi zinavyoendelea kwenye mgodi.
IMEANDALIWA NA MADUKAONLINE
SAKATA la
watu wawili wanaodaiwa kupigwa na raia wa kigeni wa China akiwemo
aliyelazwa katika Hospitali teule ya Rufaa ya Mkoa wa Geita limechukua
sura mpya baada ya kubainika chanzo chao cha kupigwa ni kuiba mawe
yanayodhaniwia kuwa na dhahabu na maji walipokuwa wakifanya kazi katika
mgodi wa dhahabu unaomilikiwa na kampuni ya RZ uliopo katika kijiji
cha Mawemeru, Mkoani Geita na siyo kutokana na madai
kupandishwa mishahara.
Tukio
hilo limetokea Januari 19 wakati wa zamu ya usiku baada ya mfanyakazi
Benedict Lumimi Maduhu kudaiwa kukamatwa akiwa na mawe yanayodhaniwa
kuwa na dhahabu ndani ya mgodi huo wakati akiwa zamu usiku na baada ya
kukamatwa rafiki yake wa karibu, Elisha
Silivester [26] ambaye naye anatuhumiwa kwa kuiba maji alifanikiwa
kukimbia hadi kituo cha polisi cha Nyarugusu kutoa taarifa kuwa yeye na
mwenzake walikuwa wakipigwa na wachina baada ya kudai waongezewe
mshahara.
Akithibitsha
tukio hilo kamanda wa polisi mkoa wa Geita Mponjoli Mwabulambo amesema
wafanyakazi Bedeicto Lumimi Maduhu walikamatwa na polisi kutoka ndani
ya mgodi huo baada ya kukuta tayari amekamatwa na kufungwa kamba na
wafanyakazi wengine wa mgodi huo tayari kwa kumpeleka kituo cha polisi
cha Nyarugusu pamoja na mawe yanayodaiwa kuwa na dhahabu .
Ameongeza
kuwa Elisha Silvesta anayedaiwa kuiba maji yeye ndiye aliyekimbia na
kutoa taarifa kituo cha polisi baada ya kufanikiwa kutoroka kabla ya
kukamatwa na polisi baada ya kufika eneo la tukio waliwachukuwa
watuhumiwa Benedicto pia wafanyakazia baadhi wa mgodi huo hadi kituo
cha polisi kwa mahojinao ikiwa ni pamoja na kuwahoji baadhi ya
wafanyakazi wa mgodi huo akiwemo Elisha mwenywe.
”Taarifa
rasmi za uchuguzi ni kuwa chanzo cha kupigwa kwao ni kutuhumiwa kwa
wizi wa mawe yanayodhaniwa kuwa na dhahabu na maji kama nilivyoeleza
sisi kama polisi pia baada ya kutokea malalamiko hayo kutoka kwa
watuhumiwa pia wanaotuhumiwa tulichukua jukumu la kuwakamata na
kuwahoji na kinachoendelea sasa ni mchakato wa kukusanya ushahidi kwa
hatua za kisheria hivyo chanzo ni cha wao kupigwa ni kutuhumiwa na siyo
madai ya nyongeza za mshahara”alidai Mponjoli.
Hata hivyo polisi imebainisha wazi kuwa zipo changamoto kwa baadhi ya watu kujenga hoja zinazolenga kujipatia
fedha
kutoka kwa wachina kwa kujenga hoja ya kupigwa na kujeruhiwa vitendo
alivyodai polisi haina budi kuyafanyia kazi kwa umakini madai hayo kwa
vile tayari ipo mifano ya matukio ambayo yaliwasilishwa lakini yakaisha
kwa walalamikaji kudai pesa na kutelekeza kesi zao.
Ametoa
mfano tukio lililtokea julai 6 mwaka jana la Masanja Shilomero[25]
mkazi wa kijiji Nyamitondo kudai kushambuliwa na wajiri wake ambao ni
raia wa china na kufunguliwa kesi namba CC/278/2016 mlalamikaji
aliitelekeza kesi hiyo baada ya kudaiwa alikuwa ameomba na kupewa fedha
kutoka kwa walalamikiwa na kuitelekeza kesi yake.
Kesi
hiyo kushindwa kuendelea na siyo kwamba imetelekezwa na polisi,na tukio
jingine amelitaja kuwa ni mchimbaji Richard Kasubi anayelalamikiwa na
baadhi ya watu wanaodaiwa kufanya kwake kazi ya kushusha mifuko ya
saruji kutoka katika gari kuiweka katika
ghala
lake badaye walidai kudhurika hata hivyo tayari inadaiwa walilipwa
pesa na mlalamikiwa huyo baada ya kutaka malipo kwa ajili ya matibabu na
baada ya kiasi cha shilingi 500,000 wanachodaiwa kupewa kukimaliza
walianza tena kudai upya na hivyo kuibua mgogoro.
kutokana
na uwepo wa mazingira ya aina hiyo polisi wanatakiwa kufanya kazi kwa
umakini ili kutenda haki kwa pande zote na kuwa Benedicto na wenzake
tayari amefunguliwa kesi ya wizi wa mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu
katika kituo cha polisi cha Nyarugusu na upelelezi wake unaendelea
ikiwemo wanaodaiwa kuwapiga nao wamefunguliwa kesi na inachunguzwa.
Awali
akizungumzia matukio hayo Meneja wa mgodi huo wa RZ Gui Xue Liu kupitia
msemaji wa kampuni hiyo Francis Beatus Kiganga amesema vitendo vya wizi
kwa wafanyakazi wanavyofanya na kisha kuwageuzia kibao kunaweza
kuwakatisha tama kuwekekeza katika sekta hiyo ya madini kwani imekuwa
ikiwapa usumbufu mkubwa.
Amesema kwa kawaida wao wamekuwa wanapowakamata watuhumiwa huamua kuwafukuza kazi badala ya kuwapeleka
kwenye
vyombo vya sheria ili kuepuka kupoteza muda na usumbufu na watuhumiwa
kutumia mwanya huo huwageuzia kibao hatua waliyodai inaonekana
kuwaathiri na kuiomba serikali kulifanyia kazi kwa umakini wimbi hilo la
wachina kutuhumwia kupiga watumishi.
Mganga wa
zamu katika hospitali hiyo Elias Hambuhambu amethibitisha juzi jioni
kwa Elisha Sivesta kulazwa hospitalini hapo kwa madai ya kupigwa na kuwa
hata hivyo hali yake ilikuwa inaendelea vizuri na alikanusha uwepo
uvumi wa kujeruhiwa sehemu za siri za majeruhi huyo kwani alikuwa
amewekewa mpira wa haja ndogo kama hatua ya kawaida kwa wagonjwa
wanaolazwa wanaokuwa na madai ya kusikia maumivu ya mwili.
Baadhi ya
wafanyakazi wa mgodi huo wakiwemo Amani Silivesta na Annicent Masanja
walidai mwenzao elisha aliondoka kwenda kuropiti Kituo cha polisi
akijihami baada ya Benedicto kukamatwa akiwa na mawe yanayodhaniwa kuwa
na dhahabu wakati alipokuwa zamu ya usiku na waliondoka na Polisi baada
ya yeye kwenda kutoa taarifa na wakati huo wote hakuwa amepigwa na
madai ya kupigwa yamejitokeza siku mbili baada ya kutokea uhalifu huo
hivyo kuibua sintofahamu.
Akizungumzia
tuhuma hizo Elisha Silvesta akiwa wodini alimolazwa juzi katika
hopitali teule ya mkoa wa Geita alikiri kuwa chanzo cha wao yeye na
Benedicto kupigwa ni kutuhumiwa yeye kuiba maji na mwenzake Benedicto
kuiba mawe yanaodhaniwa kuwa na dhahabu na baada ya kufanikiwa
kukimbia alikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi Nyarugusu kuwa
mwenzake Benecto Lumimi Maduhu alikuwa amefungwa kamba akipigwa bakora
na wachina ili kujihami
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269