Taasisi ya Eurasia Group imetangaza kuwa Rais Donald Trump wa Marekani ndiyo hatari kubwa zaidi kwa usalama na amani ya dunia.
Katika ripoti yake ya kila mwaka inayochunguza na kufanya
tathmini ya hatari zinazokabili usalama na amani ya dunia iliyotolewa
kwenye Mkutano wa Usalama wa Munich, taasisi ya Eurasia Group imesema
kuwa, Rais wa Marekani Donald Trump ndio hatari kubwa zaidi ya usalama
wa dunia.
Uchunguzi wa taasisi hiyo unasema, Trump anachukua hatua zake kwa
lengo tu la kutimiza maslahi ya Marekani bila ya kujali taathira zake
mbaya kimataifa.
Watafiti wa Eurasia Group wamesema katika ripoti hiyo kwamba, Rais
Donald Trump wa Marekani ni mtu mwenye mielekeo ya upande mmoja.
Ripoti ya Eurasia Group imesema kuwa, Donald Trump anataka
kudhibiti watu lakini makampuni ya teknolojia yanataka uhuru na kulindwa
taarifa za watumiaji wao.
Mkutano wa Usalama wa Munich ulianza kazi zake tarehe 17 Februari
ukihudhuriwa na wawakilishi wa nchi nyingi duniani ikiwemo Marekani
yenyewe.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269