Gambia imetengua uamuzi wa kujiondoa katika Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Masaa machache tu baada ya safari ya Boris Jonhnson, Waziri wa
Mambo ya Nje wa Uingereza nchini Gambia, viongozi wapya wa nchi hiyo
wametangaza kuwa, nchi hiyo itaendelea kuwa mwanachama katika Mahakama
ya Kimataifa ya Jinai (ICC).
Novemba mwaka jana aliyekuwa rais wa Gambia, Yahya Jammeh alitangaza
habari ya kujiondoa nchi yake katika mahakama hiyo. Jammeh aliituhumu
mahakama ya ICC kuwa inawaandama viongozi wa nchi za Kiafrika wakiwemo
maafisa wa Gambia yenyewe.
Yahya Jammeh pia aliiondoa Gambia katika Jumuiya ya Madola,
Commonwealth inayoongozwa na Uingereza na kutangaza kuwa, taasisi hiyo
ni ukoloni mamboleo.
Rais mpya wa Gambia, Adama Barrow ambaye aliwahi kuwa mlinzi wa duka
nchini Uingereza, ametangaza kuwa, ataimarisha uhusiano wa nchi hizo
mbili na kwamba nchi hiyo itarejea tena katika Jumuiya ya Madola.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269