Dikteta aliyepinduliwa madarakani huko Misri amesisitiza kuwa visiwa vya Tiran na Sanafir ni milki ya nchi hiyo.
Hosni Mubarak Rais wa zamani wa Misri aliyepinduliwa madarakani
amesisitiza katika ujumbe wa sauti akiwahutubu wananchi katika
kumbukumbu ya kutimia mwaka wa sita tangu apinduliwe madarakani nchini
humo kuwa kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa na mahakama ya nchi hiyo
visiwa viwili vya Tiran na Sanafir ni mali ya Misri.
Saudi Arabia na Misri zinahitilafiana kuhusu umiliki wa visiwa hivyo viwili vilivyopo kaskazini mwa bahari Nyekundu.
Saudi Arabia na Misri zinahitilafiana kuhusu umiliki wa visiwa hivyo viwili vilivyopo kaskazini mwa bahari Nyekundu.
Itakumbukwa kuwa Cairo mwaka iliafiki kuipatia Saudi Arabia visiwa
hivyo viwili kufuatika makubaliano yaliyofikiwa kati ya nchi mbili hizo;
na mkabala na hatua hiyo; Wasaudia pia wanapaswa kuwekeza katika uchumi
wa Misri, hata hivyo mapatano hayo yalibatilishwa na mahakama ya
Misri.
Wananchi wa Misri wamekuwa wakiandamana pakubwa katika mji mkuu Cairo na katika maeneo mengine ya nchi kulalamikia hatua hiyo ya serikali ya kuipatia Saudia visiwa vyao. Watu zaidi ya 200 wametiwa mbaroni na wengine kadhaa kuhukumiwa vifungo jela kwa kosa la kushiriki katika maandamano hayo.

No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269