Mkurugenzi wa Sensa
na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim
Kwesigabo, akizungumza katika mkutano na waandishi wa habari wakati
akitoa taarifa kuhusu mfumuko wa bei wa mwezi Januari 2017 jijini Dar es
Salaam leo. Kulia ni Meneja Idara ya Takwimu za Ajira na Bei, Ruth
Minja.
Waandishi wa habari wakichukua taarifa hiyo.
Wanahabari wakiwa kazini.
Mkutano na wanahabari ukiendelea.
Na Dotto Mwaibale
MFUMUKO wa Bei wa mwezi Januari 2017
unaopimwa kwa kipimo cha mwezi umeongezeka kwa asilimia 0.8
ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.7 ilivyokuwa mwezi Desemba
2016.
Hayo yamebainishwa na Mkurugenzi wa
Sensa na Takwimu za Jamii wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) wakati
akitoa taarifa hiyo kwa waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo.
"Fahirisi za bei zimeongezeka hadi 105.92 mwezi Januari 2017 kutoka 1-05.04 mwezi Desemba 2016" alisema Kwesigabo.
Alisema kuongeza kwa fahirisi za bei
kumechangiwa na kuongezeka kwa bei za baadhi ya bidhaa za vyakula na
bidhaa zisizo za vyakula.
Alitaja baadhi za vyakula zilizochangia
kuongezeka kwa fahirisi ni pamoja na mahindi kwa asilimia 6.3, ndizi za
kupika kwa asilimia 5.8, magimbi kwa asilimia 5.3 na viazi vitamu kwa
asilimia 6.5.
Alisema kwa upande mwingine baadhi ya
bidhaa zisizo za vyakula zilichochangia kuongezeka kwa fahirisi ni
pamoja na mkaa kwa asilimia 3.2 na majokofu kwa asilimia 2.4.
Kwesigabo alisema thamani ya shilingi ya
Tanzania hupima badiliko la uwezo wa shilingi ya Tanzania katika
kununua bidhaa na huduma zilezile za mlaji ambazo shilingi ya Tanzania
ingeweza kununua katikavipindi tofauti.
"Ikiwa fahirisi za bei za Taifa
zinaongezeka, uwezo wa shilingi ya Tanzania katika kununua bidhaa na
huduma hupungua" alisema Kwesigabo.
Alisema uwezo wa shilingi 100 ya
Tanzania katika kununua bidhaa na huduma umefikia shilingi 94 na senti
42 mwezi Januari, 2017 ikilinganisha na shilingi 95 na senti 20
ilivyokuewa mwezi Desemba 2016.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269