Mawaziri wa mambo ya nje kutoka kundi la mataifa 20
duniani wamekuwa wikikutana katika mji mkuu wa zamani wa Ujerumani Bonn
kujadili mizozo ilioko hivi sasa duniani na njia za kuzuwiya mizozo ya
baadae
Mawaziri wa mambo ya nje kutoka katika mataifa 20 duniani yenye
maendeleo makubwa ya kiuchumi na yale yanaoinukia wamekuwa wikikutana
katika mji mkuu wa zamani wa Ujerumani Bonn tokea hapo jana kujadili
mizozo ilioko hivi sasa duniani na njia za kuzuwiya mizozo ya baadae
wakati huku kukiwa na hali ya mashaka miongoni mwa washirika na mahasimu
juu ya mwelekeo wa sera ya kigeni ya Marekani.
Mwanadiplomasia
mkuu wa Ujerumani ambaye ni mwenyeji wa mkutano huo wa siku mbili mjini
Bonn amedokeza kwamba kuchaguliwa kwa Rais Donald Trump kunapaswa kuwa
wito wa kuizinduwa Ulaya iwapo bara hilo linataka kujiandaa kukabiliana
na changamoto zinazokuja.
Waziri huyo wa mambo ya nje wa
Ujerumani Sigmar Gabriel ameliambia gazeti la Ujerumani la Frankfurter
Allgemeine kwamba Umoja wa Ulaya unahitaji mageuzi iwapo inataka
izingatiwe kwa umakini na mataifa yenye nguvu duniani kama vile
Marekani,Urusi na China.
Gabriel amesema na " Kwa miaka mingi
tumekuwa tukiamini kwamba maisha yetu yangelindwa vizuri zaidi na
Wamarekani".Gabriel alikuwa akikusudia udhibiti wa serikali ya Marekani
kwa mataifa ya magharibi kitamaduni, kidiplomasia na kijeshi baada ya
kumalizika kwa Vita Vikuu vya Pili vya Dunia.
Kutetea maadili
Waziri wa mambo ya nje wa Ujerumani Sigmar Gabriel.
Gabriel
amedokeza kwamba wakati umefika kwa wananchi wa Ulaya kuachana na dhana
ya kanda yao kuwa ya raha na kusimama kidete kutetea maadili yao
ikibidi hata kwa nguvu za kijeshi bila ya kutegemea msaada wa
Marekani.Amesema kufanya hivyo kutasaidia kushughulikia mashaka
yanayozidi kuongezeka juu ya Umoja wa Ulaya kulikopelekea kufufuka kwa
siasa za sera kali za mrengo wa kulia katika miaka ya hivi karibuni.
Mazungumzo
rasmi miongoni mwa nchi hizo za kundi la mataifa 20 yenye maendeleo ya
viwanda na zile zinazoinukia kiuchumi yanalenga kile kinachojulikana
kama malengo ya maendeleo endelevu 17 ambayo jumuiya ya kimataifa
iliyakubali yatimizwe kufikia mwaka 2030.
Suala la vita vya Syria
vilivyodumu miaka sita linatazamiwa kuhodhi jukwaa Ijumaa (17.02.2017)
na baadae mada ya namna ya kulisaidia bara la Afrika kukabiliana na
changamoto mbali mbali zinazokwamisha maendeleo yake itapewa kipaumbele.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269