Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo wakati wa uhai wake
Rc Mongela akimpa pole Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akimpa pole MD Kayombo
Na Mathias Canal, Mwanza
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela ameongoza mamia ya wananchi waliojitokeza
kijijini Misasi, Wilaya ya Misungwi Mkoani Mwanza kwa ajili ya kusindikiza
safari ya mwisho ya kurejea mavumbini kwa utimilifu wa vitabu vitakatifu vya
Dini Mzee Anton Raphael Kayombo.
Mkuu
wa Mkoa wa Mwanza Mhe John Mongela akiteta jambo na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi Ndg Eliud Mwaiteleke kulia ni Mbunge
wa Jimbo la Nyamagana Stanslaus Mabula
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mhe Ally Happi akisaini kitabu cha wageni kabla ya mazishi
Rc Makonda akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Rc Mongela alisema kuwa kifo cha Mzee Kayombo kimeacha alama kubwa Duniani
kwa ufanisi mkubwa alioufanya akiwa hai ambapo pia ni alama kubwa ya taswira ya
fikra huru zitakazoishi kwa Yale aliowaasa wananchi katika maelekezo mbalimbali
ikiwemo ushauri katika serikali.
Mongela aliyeambatana na mkewe katika mazishi hayo amewapongeza wananchi
wote kwa kujitokeza mwenye mazishi hayo sambamba na kuwasihi kuendelea kutoa
mshikamano kwa serikali katika majukumu mbalimbali ikiwemo kusimamia na
kudumisha umoja waliouonyesha katika mazishi ya Mzee Kayombo.
Dc Happi akiaga mwili wa marehemu Mzee Kayombo
Mstahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mhe Benjamini Sitta akisaini kitabu cha wageni mara baada ya kuwasili kijijini Misasi
Kwa upande wake Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe Paul Makonda alisema kuwa
Mkoa wa Mwanza umepoteza mtu muhimu ambaye atakumbukwa kwa kazi njema
alizozifanya wakati wa uhai wake ikiwemo kuwa mlezi bora wa familia yake na
hatimaye kupatikana kwa kiongozi bora na mwenye weledi katika utendaji kazi.
Akizungumza kwa niaba ya kundi la mtandaoni (Watsup) la The Impossible is
Impossible Bwana Steve Nyerere ametoa pole kwa Mkurugenzi wa Ubungo Ndugu John
Lipesi Kayombo kwa kuondokewa na Mzee wake ambaye ni Mlezi wake tangu akiwa mdogo
sambamba na kuwasihi wananchi kuendeleza mshikamano na kupendana.
Rc Makonda akitoa salamu za pole kwa niaba ya Viongozi wengine alioambatana nao kutoka Jijini Dar es salaam
Mkurugenzi wa Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo akitoa salamu za shukrani akiwa na Mkewe
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo Ndg John Lipesi Kayombo
alisema kuwa Mzee wake Hugo atakumbukwa kwa mambo mbalimbali aliyoyafanya
wakati wa uhai wake pindi alipokuwa kazini ikiwa ni pamoja na kupanda miti
katika shule zote alizofundisha, Ujenzi wa shule wakati huo, pia atakumbukwa
kwa kuhamasisha ujenzi wa Zahanati ya Misasi.
Ameeleza kuwa Marehemu Mzee Antony Raphael Kayombo alikuwa anasumbuliwa na
ugonjwa wa kibofu cha mkojo ambao ulianza ghafla tarehe 29/1/2017 na kupelekwa
katika hospital ya Misasi, Baadae hospitaliti ya Sekou Ture na mwishowe
Hospitali ya Bugando ambapo alifanyiwa upasuaji ambapo hata hivyo hali yake
iliendelea kudhoofika mpaka mauti ilipomkuta tarehe 4/2/2017 majira ya saa
mbili usiku.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269