Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini Rogers Sianga
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
JAJI Mkuu
anatarajia kupokea orodha ya majina ya mahakimu na majaji ambao
wamevuga kesi za watu wanaotuhumiwa kujihusisha na dawa za kulevya.
Hayo
ameyasema jana Kamishina wa Mamlaka ya Kudhibiti Dawa za Kulevya nchini
Rogers Sianga wakati wa mkuatano wa viongozi mbalimbali wa kitaifa na
waandishi wa habari ulioandaliwa na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul
Makonda kwa ajili kupambana na dawa za kulevya.
Sianga
amesema kuwa kesi zimevurugwa na mahakimu na majaji. hivyo wale wote
wanaohusika watashitakiwa na hata wawe na mali ambazo wamezipata kwa
biashara hiyo zitataifishwa.
Amesema
kuwa watazunguka katika maeneo mbalmbali ya jiji la Dar es Salaam ili
kuhakikisha mtandao huo unapatikana na kwenda hata Zanzibar na mbinu
zote wanazijua katika kufanya biashara hiyo.nae Mkuu wa Mkoa wa Dar es
Salaam, Paul Makonda amemkabidhi orodha ya majina 97 wanaojihusisha na
dawa za kulevya na kuongeza kuwa moto umewashwa dhidi ya watu
wanaojihusisha na dawa za kulevya.Amesema kuwa kuna nyumba 200
zinajihusisha na kufanya biashara ya madawa ya kulevya hapa jijini
ambapo wote hao watafikiwa katika operesheni.
Nae
Mohamed Khalid TID , amesema kuwa sasa ni mnyama ambae yuko tayari
kupambana nawatu wanaouza pamoja na kutumia dawa za kulevya na amerudi
kwa kufanya kazi na kuongeza kuwa kuimba hakuhitaji dawa za kulevya.
Katika mkutano huo watu wawili wametakiwa kufika katika Kituo cha Polisi kati ambao ni Chidi Mapenzi, Ayuob Mfaume Kiboko.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269