Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam,Isaya Mwita, akisalimiana
na Mwenyeji wake, Daluwesh Dume (katikati) kwenye hafla ya sherehe ya Maulid ya kuzaliwa,
Mtume S.A.W iliyofanyika Mtaa wa Da Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es
Salaam jana.
Mstahiki Meya wa Jiji la Dar es Salaam, Isaya
Mwita akizungumza katika hafla ya ufunguzi wa sherehe ya Maulid ya kuzaliwa Mtume
Mohamed (S.A.W) iliyoandaliwa na Muumini wa Dini hiyo Daluwesh Dume iliyofanyika
Mtaa wa Ada Estate eneo la Kinondoni jijini Dar es Salaam jana. Katikati ni
Diwani wa Kata ya Kinondoni, Mustapha Muro.
NA ELISA SHUNDA,DAR
MEYA wa jiji la Dar es Salaam, Isaya Mwia amewaomba
Mashehe na Wazee wa jiji kumuunga mkono katka shughuli anazofanya ili kuweza
kutatua changamoto zilizopo katika jiji hili.
Meya Isaya ametoa kauli hiyo jiji hapa jana wakati wa
maulidi ya kusherehekea kuzaliwa kwa Mtume Muhammad Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam
ambapo pamoja na mambo mengine amesema kwamba jiji la Dar es Salaam bila dua za
waze, mashehe na viongozi wote wadini huwezi kuliongoza kutokana na changamoto
zilizopo.
“ Najua changamoto zilizopo kenye jiji hili ni nyingi wazee
wangu naomba mnisaidie sana, peke yangu siwezi, dua zenu na ushauri wenu ndio
unaweza kunisaidia mimi kufanya mambo mazuri” na wananchi wakaishi kwenye mazingira
wanayopenda” amesema Meya Isaya.
Leo mimi nikiwa na kiburi kweu kwa ajili ya madaraka haya
ambayo nyie ndio mlionipa, sitaweza kutatua changamoto hata moja, zipo changamoto
za kimiundombinu ya elimu, na nyingine, ambazo zote zinahitaji kupatiwa
ufumbuzi, nawaombeni sana waze wangu mnipe baraka zenu” aliongeza.
Akizungumzia suala la
maadili Meya Isaya amesema wazazi hawana budi kuwasaidia walimu, serikali na
viongozi kwa ajili ya malezi bora hususani wakiwa shuleni.
Amesema ni jambo la ajabu na mtihani mkubwa kwa walimu ikiwa
mzazi atakuwa mstari wa mbele kumnunulia mwanae simu hali yakuwa yupo masomoni
jambo ambalo linafanya ashindwe kuzingatia masomo na badala yake kushinda
kwenye mitanda ya kijami.
“ Leo hi mzazi unapomnunulia mwanao simu wakat unajua kabisa
anasoma, huu simtihani jamani, leo hii mzazi unaposhindwa kufuatilia maendeleo
ya mtoto wako shuleni huu simtihani jamani, nawaombeni sana tusaidiane kulea
watoto wetu” ameongeza Meya Isaya.
Aidha Meya Isaya amewataka vijana kuacha tabia a kukaa
vijiweni badala yake wajikite kwenye kufanya kaz, huku akiwaaka wazazi
kutokufumbia maco vijana wao aba hatawai kujishuguisha.
Amesema vijana waliowengi hawataki kujishugulisha na
badala yake husubiri kila abacho wazazi wa hutafuta jamo abalo humjengea kijana
mazingira ya watto kuanza kugawaa mali kaba ya wazazi hawaja toweka duniai.
“ Wazazi msiwavumilie vijana wenu ambao wanasubiri
nyie muende mkatafute wao waje wale, leo hii nyumbani unakuta baba, au Mama
anapishana na kijana wake ambaye angekuwa anajitegemea mwenyewe, lakini
kuendelea kuishi nao nyumbani mnataka kuwaongezea umasikini” amesema Meya Isaya.
Matokeo yake, unakuta kijana anasema Baba unakufa
lini, am wanaanza kugawana mali ambazo mmetafuta nyinyi, kabla hata bado hamjatoweka
duniani, jambo hili jamani sio mtihani ndugu zangu?, lazima tuwalee watoo wetu
kwenye misingi ya kuwaeleza kwama dawa ya kupambana na umasikini kufanya kazi” amesisitiza.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269