Shirika la misaada la kiarabu la Hilali nyekundu nchini Syria ,
linasema shambulio la kombora katika mji unaodhibitiwa na serikali wa
Aleppo, limemuuwa mmoja wa watumishi wake wa kujitolea na raia wengine
wawili ambao wakihitaji msaada. Shirika hilo linasema kombora
liliangukia kwenye kituo cha usambazaji misaada katika eneo la
Hamadaniya na kuwajeruhi watu wengine saba wafanyakazi wa Hilali
nyekundu. Shirika la Kimataifa la Msalaba Mwekundu limethibitisha tukio
hilo.Majeshi ya serikali ya Syria yaliwashinda wapiganaji waasi mjini
Aleppo mwezi Desemba baada ya miaka kadhaa ya mapigano makali, lakini
upinzani ungali ukiyashikilia baadhi ya maeneo kwenye vitongoji vya mji
huo. Mapigano yameendelea katika maeneo hayo ya Aleppo na kwengineko
nchini Syria licha ya usimamishaji mapigano uliofikiwa Desemba 30.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269