Breaking News

Your Ad Spot

Feb 18, 2017

WATUHUMIWA 326 WAKIWEMO WA DAWA ZA KULEVYA HEROINE WANASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI KIGOMA

NA MAGRETH MAGOSSO,KIGOMA
JUMLA ya watu 326 wanashikiliwa na Polisi mkoani Kigoma kwa tuhuma mbalimbali wakiwemo wahamiaji haramu 226 waliokutwa na dawa za kulevya aina ya Heroine, 44 kwa tuhuma za kuhusishwa na mashamba ya bangi, 54 kukutwa na mitambo ya kutengeneza na mmoja kukutwa na bunduki aina ya gobore.

Akifafanua, Kamanda wa Polisi mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema kwa kipindi cha wiki moja katika msako endelevu wa watumiaji na wasambazaji wa dawa za kulevya upande wa wilaya ya Kigoma mjini walikamata kete  tano za heroine na bangi kete 191 na gramu 10, wakati wilaya ya Kasulu walikamata shamaba la bangi lenye ukubwa wa robo heka  na gramu 500 za bangi, wilaya ya Kibondo wamekamata miche 10 ya bangi, Kakonko miche 60 , kilo moja na gramu 500.

Alisema wamekamata jumla ya lita 300 ya pombe aina ya gongo ambapo wilaya ya kigoma wamekamata lita 229,kasulu 25, kibondo lita 15, kakonko lita 31, manyovu lita 15,huku wakishikilia mtambo mmoja wa kutengeneza pombe hiyo wilayani kibondo na wilaya ya uvinza mmoja amekutwa na silaha aina ya gobore
Aidha aliwapongeza wananchi kwa kutambua umuhimu wakutoa tarifa ya uwepo wa wahalifu na wahamiji haramu wenye historia ya uhalifu hasa wanaotoka  nchi ya burundi na kuwasisitiza wananchi wasiogope kutoa tarifa zenye maslai mapana ya taifa lao.

Kamanada Mtui alisema watuhumiwa hao watapelekwa mahakamani kujibu tuhuma zinazowakabili mara tu ya upelelezi kukamilika ambapo kwa sasa wana kesi moja ya heroine,kesi 8 wahamiaji haramu,kesi 12 pombe ya gongo,bhang kesi 9 na silaha kesi mojatu.

No comments:

Post a Comment

Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269

Post Top Ad

Your Ad Spot

Pages