Basi la
Ally's Star Gufl Air lenye namba za usajiri 514 ANW likitoka Mwanza
kwenda Tabora, limepata ajali asubuhi ya leo majira saa moja katika
kijiji cha Mwazenze wilayani Misungwi Mwanza mara baada ya kugongana uso
kwa uso na lori la mizigo na kuacha njia.
Kwa
mujibu wa maelezo ya abiria waliokuwa wamepanda kwenye basi hilo
wamesema chanzo cha ajali hiyo ni mwendokasi wa dereva alipokuwa
akijaribu kuovateki gari iliyokuwa mbele yake pasipokujua mbele yake
zaidi kuna nini, ndipo basi hilo likagongana ghafla na lori la Azam lililokuwa limebeba unga wa ngano.
Katika
ajali hiyo, hakuna mtu aliyefariki wala kuumia zaidi ya mtu mmoja kupata
mshituko wa mguu. Dereva alitoweka mara tu baada ya ajali hiyo kutokea. (PICHA NA MASENGWA BLOG BLOG)
Lori la mizigo lililogongana na basi hilo likiwa limeharibika baada ya ajali
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269