Elias Nawera. |
Na Brandy Nelson
Mkurugenzi
Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe mkoani hapa,Elias Nawera
ambaye ameingia mgogoro na madiwani wake, ameibuka na kutoa msimamo wake
kwamba atafanya kazi kwa mujibu wa sheria, taratibu na kanuni za
utumishi wa umma na si kwa matakwa ya wanasiasa.
Hivi
karibuni Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Songwe wakiongozwa na
Mbunge wa Jimbo la Songwe, Phillipo Mulugo walidai kutoridhishwa na
hawana imani na utendaji kazi wa mkurugenzi huyo kwenye kikao chao
kilichoitishwa kwa dharula kwa lengo la kumjadili na kumuazimia kumfuka
kazi.
Akizungumza
juzi , Nawera alisema kuwa amepelekwa kwenye halmashauri hiyo kwa ajili
ya kuwatumikia wananchi na siyo kumtumikia mtu mmoja mmoja kwani
kufanya hivyo ni kukiuka misingi ya utawala bora.
"Unajua
baraza la madiwani ni wawakilishi wa wananchi na ni siasa, na siasa
mara nyingi ilivyo ni nani kapata nini wakati gani vipi, kimsingi ndiyo
siasa, wilaya yetu ni mpya na kuna watu wanataka kufanya kazi kwa
namna walivyokuwa wamezoea kufanya mambo yao, kitu ambacho siwezi
kukubaliana nacho hata siku moja,"alisema.
Alisema
tangu alipofika katika halmashauri hiyo Septemba mwaka jana, alikuta
mazoea ya watu kama wana ufalme kana kwamba Serikali haipo, hivyo
yupo Songwe kufanya kazi kimfumo wa kiserikali na siyo kumtumikia mtu
mmoja mmoja ambapo jambo hilo limekuwa likikwaza watu.
"Mfano
kwenye kikao cha halmashauri nililazimishwa kumpa mtu kazi kwa
jina,kufanya biashara na mtumishi wa halmashauri ,nikiuke sheria ya
manunuzi kwa kusema sheria nini,vitu ambavyo sikubaliani navyo kwani
kufanya hivyo nikukiuka sheria,taratibu na misingi ya utawala bora
".alisema
Mkurugenzi
huyo alisema amekuwa akienda vijijini kwa ajili ya kufuatilia
utekelezaji wa miradi ya maendeleo ikiwa ni pamoja na kusikiliza kero za
wananchi lakini amekuwa akizuiwa kufanya hivyo na kuambiwa abaki
ofisini.
"Nimewahi
kukatazwa nisiende vijijini,mimi ninajua rais amenileta huku nitumikie
watu na Ilani yenyewe ya chama cha mapinduzi inasema lazima twende
chini tufanye kazi na watu, kwa hiyo ukiniambia kitu tofauti na hicho
miongozo, sheria kanuni na taratibu mimi sitokusikiliza kwa sababu
nitataka kutumikia wananchi na kumsikiliza yule aliyenileta.'alisema
Alisema
hata Mkuu wa Mkoa wa Songwe, Chiku Galawa mara nyingi amekuwa
akiwaagiza watendaji kutoka ofisini na kwenda vijijini kwa wananchi,
kwani pia kuna watumishi ambao wapo huko na wanahitaji huduma lakini
hawana uwezo wa kufika wilayani hivyo hutumia fursa hiyo kuwasikiliza
mahitaji yao.
Aidha
alisema ameshangazwa na utaratibu wa Mkurugenzi kutakiwa kutoa taarifa
katika ofisi ya mbunge au kwa katibu wa mbunge anapotaka kwenda
vijijini kufanya kazi.
"Ukisimamia
kwenye msimamo wa kufuata misingi ya sheria kanuni na taratibu za
utumishi wa umma hapo ndipo unaonekana haufai,unakiburi au huna
adabu"alisema
Akizungumzia
mgogoro huo, Mkuu wa Mkoa wa Songwe Chiku Galawa alisema ni kitu cha
kawaida katika utendaji kazi kwani hata katika familia hali hiyo hutokea
na kwamba amewataka watumishi wa halmashauri hiyo kufanya kazi kwa
utulivu na kusahau yaliyopita.
Chanzo Gazeti la Mwananchi.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269