Makonda
amezitembelea nyumba hizo katika Kata ya Buguruni kwa Mnyamani na Tabata
, akiwa na vikosi vya ulinzi na usalama ambapo ameshuhudia maafa
makubwa yakiwemo ya baadhi ya watu kupoteza mali pamoja na nyumba zao
kujaa maji na ameagiza kubomolewa kwa nyumba 36
ambazo zipo kwenye maeneo hatarishi ya mabondeni ikiwemo bonde la mto
msimbazi, hali ambayo imepeleka kaya nyingi kukumbwa na mafuriko.
Kufuatia
mvua zilizoanza kunyesha tarehe nane mwezi huu, zimepelekea kuleta
maafa ikiwemo kifo cha mtu mmoja kilichotokea eneno la jangwani Jijini
Dar es Salaam, pamoja na watu wengi kupoteza makazi, jambo ambalo
limemgusa RC Makonda na kufikia uamuzi huo wa kuiomba Halmashauri ya
Ilala kuanza zoezi hilo la ubomoaji mara moja.
RC
Makonda amesema kuna watu ambao tayari wamelipwa pesa kuhama maeneo
hayo lakini cha ajabu wengine hawajaondoka na wengine wamewapangisha
watu wengine kwenye maeneo hayo hatarishi, jambo ambalo serikali yake
haiwezi kufumbia macho na kuagiza kubomolewa kwa nyumba hizo.
Pia
amewataka wale ambao hawajahakiki taarifa zao kuhusu kupewa hifadhi
baada ya nyumba zao kubomolewa wafanye hivyo kwa kwenda ofisi ya Mkuu
wa Wilaya ya Ilala kwa uhakiki huo.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269