Waziri
wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati), Mkuu wa mkoa
wa Pwani, Mhandisi Evarist Ndikilo (wa kwanza kushoto), Mbunge wa
Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete (wa pili kushoto), Mbunge wa Kibaha
Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa (wa nne kushoto) na Mkurugenzi Mkuu wa Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Gissima Nyamo-hanga wakifurahia
uzinduzi wa mradi wa Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA
III) katika mkoa wa Pwani. Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika
kijiji cha Msufini mkoani humo.
Na Teresia Mhagama
Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo, amezindua mradi wa
Usambazaji Umeme vijijini wa Awamu ya Tatu (REA III) katika mkoa wa Pwani
ambao utawezesha vijiji mbalimbali katika mkoa huo kupata huduma ya Umeme.
Hafla ya Uzinduzi huo ilifanyika katika kijiji cha Msufini mkoani humo na
kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa mkoa wa Pwani,
Mhandisi Evarist Ndikilo, Mbunge wa Chalinze, Mhe. Ridhiwani Kikwete na
Mbunge wa Kibaha Vijijini, Mhe.Hamoud Jumaa.
Uzinduzi wa mradi huo ulienda sambamba na utambulishaji wa Mkandarasi
atakayetekeleza sehemu ya kwanza ya Mradi huo ambaye ni kampuni ya Steg
International Services.
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269