Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa maelekezo kwa Waziri wa Maji Mhandisi
Gerson Lwenge kuhakikisha kuwa Mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo mkoani Lindi
unakamilika ndani ya miezi mine na si vinginevyo.
. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Mama Salma Kikwete mara baada ya
kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa Maji wa Ng’apa uliopo
Mkoani Lindi. Pia Mama Salma Kikwete amemshukuru Rais Dkt. Magufuli kwa kumteua
kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mbunge mteule Mama Salma
Kikwete mara baada ya kuwasalimia wananchi waliokusanyika karibu na mradi wa
Maji wa Ng’apa uliopo Mkoani Lindi.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na wananchi wa Ng’apa mara baada
ya kutembelea mradi wa Maji wa eneo hilo ambao unasuasua kukamilika. Rais Dkt.
Magufuli ametoa miezi minne kwa Mkandarasi kampuni ya Overseas Infrastructure Alliance
Private Limited ya India kuhakikisha kuwa inakamilisha ujenzi wa mradi huo na
sio kuleta visingizio.
. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Bodi
ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu ndogo Mkoani
Lindi
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza mara baada ya kumaliza mazungumzo
yake na Bodi ya Wakurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) katika Ikulu
ndogo Mkoani Lindi. Wakwanza kushoto ni Kiongozi wa Wakurugenzi hao Lekhethe Mmakgoshi
kutoka Nchini Afrika Kusini na Wakwanza kulia ni Mkurugenzi mwingine wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje
Weggoro ambaye ni Mtanzania.
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiagana na
Kiongozi wa Wakurugenzi hao kutoka (AfDB) Lekhethe Mmakgoshi mara baada ya
kumaliza mazungumzo na Bodi hiyo ya Wakurugenzi.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza jambo na Mmoja wa Wakurugenzi wa (AfDB) Dkt.Nyamajeje Weggoro mara baada ya kumaliza mazungumzo na Bodi yao Ikulu ndogo mkoani Lindi.
Sehemu
ya Mradi wa Maji wa Ng’apa mkoani Lindi ambao Rais Dkt. Magufuli ametoa miezi
minne kwa mkandarasi anayejenga mradi huo ili uweze kukamilika haraka.PICHA NA IKULU
No comments:
Post a Comment
Toa Maoni kistaarab kwa Hoja kwa faida ya wenzako. au tundikie kupitia nkoromo@gmail.com, simu 0672223269